Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Waziri Ummy akisisitiza jambo mapema leo katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo.

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WAZIRI wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kamwe hatamvumilia mtumishi katika sekta ya afya ambaye atabainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Aidha, amesema hatamvumia mtumishi yeyote wa sekta ya afya ambaye atabainika kuzungumza lugha 'mbovu' kwa mgonjwa.

Amewataka watumishi hao kujiepusha na vitendo vya rushwa hasa wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao kulingana na maadili ya utumishi wa umma.

Maagizo hayo ameyatoa Dar es Salaam leo, alipofungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ambacho kimelenga kujadili  mustakabari wa utoaji huduma za afya nchini. 
Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu, Dk. Otilia Gowelle wa kwanza kulia na wajumbe wengine wakimsikiliza kwa umakini Waziri Ummy (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.


"Ni marufuku kujihusisha na vitendo vya rushwa na ikiwa kuna mtumishi ana tabia hiyo aache mara moja kwani akibainika sheria itafuata mkondo wake mara moja," amesisitiza.

Ameongeza "Kuweni na lugha nzuri kwa wananchi, nimepokea kesi moja Hospitali ya Taifa Muhimbili, mama mmoja alinipiga kulalamika juu ya daktari ambaye bahati nzuri jina lake ninalo na nimelikabidhi kwa uongozi ili achukuliwe hatua na iwe mfano kwa wengine.

Amewataka pia kuweka kipaumbele katika kutoa elimu juu ya magonjwa yasioambukiza kwani yamekuwa yakiongezeka kila kukicha kutokana na ukosefu  elimu ya kutosha kuhusu magonjwa hayo. 
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.

Waziri Ummy amewataka kuwa mfano wa kuigwa hasa katika kufanya mazoezi,  kula lishe bora pamoja na kutoa elimu ya magonjwa mbalimbali ili kuisaidia kuondoa ongezeko la magonjwa yasioambukiza" alisema Waziri Ummy. 

Amesema kuwa ili kufikia adhima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jonh Pombe Magufuli la kujenga uchumi wa Viwanda ni lazima kuzingatia utoaji wa huduma bora za afya ili kuwa na wananchi  wenye afya ambao watasukuma gurudumu kufikia lengo hilo. 

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Taifa wa Balaza la Wafanyakazi TUGHE, Nsubisi Mwasandende amesema kuwa katika kutatua changamoto za magonjwa mbalimbali watendaji wa Wizara ya Afya wanatakiwa kuzingatia hali ya upatikanaji wa chanjo ili kuboresha huduma za afya. 

Amesema watumishi wanatakiwa kulifanyia kazi haraka  agizo la Waziri Ummy la kutokomeza vitendo vya rushwa haraka iwezekanavyo  ikiwa kama moja la adhimio la katiba ya balaza la wafanyakazi. Waziri Ummy akiimba pamoja na wafanyakazi wa Wizara hiyo wimbo wa kuhamasisha umoja wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.

Picha zote kwa hisani ya Wizara.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement