Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Image result for PREGNANCYHii ni sehemu ya pili ya ripoti hii ambako katika sehemu ya kwanza wanawake walipata nafasi ya kueleza changamoto walizokatana nazo katika safari yao hii.

Hapa tunaendelea, karibu, Imeandaliwa na Veronica Romwald, aliyekuwa Morogoro


Hivi karibuni tulishuhudia jinsi ambavyo ‘sekeseke’ hilo lilipamba moto kiasi cha baadhi ya viongozi wa serikali kuonekana waziwazi wakiwachukulia hatua wauguzi na wakunga waliodaiwa kutoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa kwa kuwaweka rumande.

Hata hivyo, ililazimu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoa tamko la kuwataka viongozi wa serikali kuziachia mamlaka zinazosimamia maadili ya kitaaluma kuwachukulia hatua watumishi hao kwa kufuata misingi ya sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

Pamoja na hayo, inadaiwa watumishi wengi wa kike wa kada hizo ndiyo ‘vinara’ wa kutoa lugha chafu kwa wajawazito tangu wanapohudhuria kliniki na hadi kipindi cha kujifungua kuliko watumishi wa jinsia ya kiume.

Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA). Feddy Mwanga anakiri kwamba wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa jamii dhidi ya baadhi ya wakunga.

“Wapo wanaotuhumiwa kutoa lugha zisizofaa na tunapopokea malalamiko tunafuatilia kwa ukaribu na ambaye anakutwa na hatia tunamchukulia hatua kwa mujibu wa sheria,” anabainisha.

Utafiti wafichua mambo

Maurice Hiza ni Ofisa katika Idara ya  Huduma na Ukunga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anasema waliamua kufanya uchunguzi wa kina juu ya malalamiko hayo.

“Tulipokea malalamiko mengi mno na tukaamua kufanya uchunguzi wetu wa kina ili kujua je ni kweli au watu walikuwa wakieneza tu uvumi, baada ya uchunguzi wetu tulibaini ni kweli wapo baadhi ya wakunga ambao hutamka lugha zisizofaa wanapokuwa wakihudumia wateja,” anasema.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubsya anasema wizara ina utaratibu maalum wa kushughulikia kero zinazowapata wafanyakazi wake.

Anasema taratibu hizo zinaendana na sheria za nchi na zimewekwa mahusus kuzishughulikia kero zozote ziwe zimesababishwa na mazingira ya kazi, wafanyakazi wenzao au watu wanaokuja kupata huduma.

“Mara nyingi tunaweza kuwa tunashughulika na watu wanaotoa huduma baada ya wafanyakazi kuja kutoa taarifa kwamba wamefanyiwa jambo fulani au mtu ameona mfanyakazi amefanyiwa jambo akatupa taarifa na sisi tunafuata utaratibu.

“Tunauliza mfanyakazi amefanyiwa jambo gani na lazima tumjue aliyefanya jambo husika, hatua hii imetusaidia mno kutatua kero mbalimbali za wafanyakazi , vile vile mahali pa kazi ni salama kwa sababu ya utaratibu tuliojiwekea wa ndugu, namna ya kuingia katika maeneo ya kazi hata wagonjwa wenyewe.

“kwa hiyo hatutegemei wakunga wanaweza kudharauliwa, kutukanwa na ndugu kwa mazingira ya kawaida ya kazi kwa sababu anaposhughulika na wajawazitokuna utaratibu wao ambao wanausimamia,” anasema.

Dk. Ulisubisya anasema hata hivyo pamekuwa na malalamiko na mengi huyapokea kutoka kwa ndugu wa wagonjwa kulalamikia huduma zinazotolewa hasa kuhusu lugha.

“Hilo tumekuwa tukilishughulikia mno kwa kuhakikisha tunakuwa na huduma rafiki katika maeneo yote,” anabainisha.

Wakunga wafunguka

Wakati jamii ikilalamika na kuwatuhumu baadhi ya wakunga kutotimiza wajibu wao kwa mujibu wa misingi ya taaluma yao.

Wakunga nao wamefunguka na kutoa yale yaliyo moyoni mwao ambapo hapa wanaeleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza na MTANZANIA Mariam Japhet, Mkunga wa Hospitali ya Ulanga mkoani Morogoro anasema amefanya kazi hiyo tangu mwaka 1990 na kwamba amekutana na mikasa ya namna nyingi.

“Nakumbuka kuna siku nilipokea mjamzito ambaye mapigo yake ya moyo nay a mtoto yalionekana kushuka mno, nilimjulisha daktari alipokuwa akimfanyia vipimo zaidi yule mama alibaini mtoto alikuwa tayari amefariki dunia.

“Alipofanyiwa upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni, alikutwa na tatizo la kichwa kikubwa, basi ndugu aliyekuwa amekuja na mgonjwa alijulishwa lakini alipokuja mumewe hakuwasilisha vizuri maelezo yale aliyopatiwa,” anasema.

Anasema hali hiyo ilisababisha baba wa mtoto husika na baadhi ya ndugu kuanza kulalamika kuwa mtoto wao alikuwa amefariki kutokana na uzembe.

“Ikabidi tutumie ujasiri kumuita baba husika na kumuonesha ule mwili wa mtoto wake alipoangalia na kuona alikuwa na tatizo la kichwa kikubwa aliamini hakukuwa na uzembe uliokuwa umefanyika,” anasema.

Muuguzi mkunga mwandamizi Agnes Mtawa ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Msajili wa Baraza la Wakunga Tanzania anasema katika miaka zaidi ya 20 aliyohudumu katika fani hiyo amepitia mambo mengi.

“Katika hospitali niliyokuwa nasimamia, kuna siku aliletwa mjamzito ambaye alifikishwa akiwa amechoka mno na bahati mbaya mtoto alifariki tukiwa zamu ya usiku tutachukua kitenge chake tukastiri mtoto.

“Ndugu walipokuja asubuhi wakabaini kitenge hakikuwepo wakadai kwamba kilikuwa kimeibiwa na wakunga tuliokuwa usiku ule, kwa haraka haraka tulikubaliana tulipe.

“Lakini tulifanya jitihada kuangalia kilienda wapi, tukakagua na kubaini kwamba tulimfungia mtoto baada ya kufariki dunia, ndugu walikuwa tayari wamekasirika hawakuwa na uchungu tena na kifo cha mtoto wao walikuwa na uchungu na kile kitenge.

“Kwa kawaida tulikubaliana kwamba mama akiletwa pale hospitalini (Muhimbili) kila kitu chake alichokuja nacho lazima kiandikwe anapoingia na anapotoka, na hatua hiyo ndiyo ilitusaidia kujua ukweli kwamba kitenge hakikupotea bali alifungiwa mtoto kumsitiri,” anasema.

Itaendelea... Usikose nakala ya gazeti la MTANZANIA ambalo nalitumikia.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement