JESHI la Nigeria limesema limewaokoa
watoto wa kike mia mbili na tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko
Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi
hiyo. Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale
waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la
Chibok.
Jeshi limesema kwamba wanawake na watoto hao wa kike
walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia
zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao baada ya
kuziharibu kambi hizo.
"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu
wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo
walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo
ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake
tisini na tatu."
Kwa
sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata hivyo,
jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi waliotekwa
katika mji wa Chibok.
"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa
wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka
nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari
watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka
jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda
unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote. "
source BBC.
Chapisha Maoni