Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
wanafunzi wakifanya mtihani.
OFISI ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
imesema Juni, mwaka huu itatangaza majina ya wanafunzi wanaotarajia kujiunga na
masomo ya Kidato cha tano
Katibu Mkuu wa TAMISEMI alisema hayo hivi karibuni
alipozungumza na MATUKIO NA MAISHA jijini Dar es Salaam lilipotaka kujua ni lini
watataja shule walizopangiwa wanafunzi hao na hatma ya shule za Serikali
zilizofungwa kutokana na ukosefu wa chakula.
“Kwa kawaida wanafunzi waliofaulu kwenda kidato cha tano
wanatakiwa kufika shule mwezi Julai… kwa hiyo TAMISEMI tunatarajia kuwatangazia
mapema kabla ya Juni 15, mwaka huu, wajue shule wanazotakiwa kwenda weze kufika
ili wakaanze masomo yao mara moja,” alisema.
Akizungumza juu ya hatma ya shule zilizofungwa hivi karibuni
alisisitiza kwamba Serikali haitambui kufungwa kwa shule hizo na kwamba
imewaagiza waajiri kuchukua hatua.
“Kufunga shule ni suala la kitaifa na ili ifungwe lazima
waajiri wajue niliwaagiza wachukue hatua
kwa wale waliofunga shule hizo,” alisema
April 13, mwaka huu akizungumza na waandishi wa habari
jijini hapa Sagini alisema fedha hizo za chakula hutolewa kwa awamu na
kukamilishwa katika kipindi cha mwaka wa fedha unaotekelezwa.
Alisema Serikali hutoa huduma ya chakula kwa shule za
sekondari za bweni na shule za msingi elimu maalum za bweni kwa kuzingatia
fedha zilizotengwa na upatikanaji wake katika mwaka husika.
Alisema kati ya Julai 2014 hadi Machi 2015, Serikali ilitoa
Sh bilioni 28.1 kwa ajili ya chakula cha wanafunzi ambazo ni sawa na asilimia
66.7 ya Sh bilioni 42.1 zilizotengwa kwa mwaka 2014/15. Kiasi kilichobaki ni Sh
bilioni 13.9 sawa na asilimia 33.23 ya fedha zilizotengwa,”alisema.
Baadhi ya shule ambazo zilifungwa ni Rugambwa, Kahororo,
Nyakato, Ihunga (Kagera), Lyamungo (Kilimanjaro), Mpwapwa, Abeid Aman Karume
(Dodoma), Kazima, Milambo, Tabora wasichana na wavulana
Chapisha Maoni