Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement



                                       Rais Pierre Nkurunziza

 BUJUMBURA

Makundi hasimu ya wanajeshi yanakabiliana katikati  ya mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
 
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
 
Redio na runinga ya taifa inang'ang'aniwa kwa sasa huku wanajeshi waaminifu kwa rais Nkurunziza ndio wanaoidhibiti.

Kwa  mujibu  wa  taarifa  ya  habari  ya  DW  mchana  huu, rais  Nkurunzinza  ametoa  tamko  fupi  kupitia  ukurasa  wa  twitter  wa  rais  akiwataka  wananchi  wa  Burundi  kuwa  watulivu.

Taarifa  ya  DW  pia  imearifu  kuwa  Mkuu wa majeshi nchini Burundi Meja Jenerali Prime Niyongabo  ametangaza  kuwa  jaribio  hilo  limefeli.

Hata  hivyo,Mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi ya Burundi Meja Jenerali Godefroid Niyombare  ambaye  ndiye  aliyeongoza  mapinduzi  hayo  amesema  kuwa  hizo  ni  propaganda  tu  za  baadhi  ya  wanajeshi  watiifu  kwa  rais  Nkurunzinza.

Niyombare  amesema  kuwa  kama  ni  kweli  mapinduzi  yamefeli, basi  rais  Nkurunzinza  arudi  nchini  leo,asiporudi leo  basi  hakuna  haja  ya  kubishana  juu ya  uwepo  wa  mapinduzi  hayo.

WAKATI huo huo, 

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya mkutano wa dharura hii leo kuijadili Burundi baada ya jenerali mwandamizi wa jeshi nchini humo kutangaza kumpindua Rais Pierre Nkurunzinza kutoka madarakani.



Ufaransa ndiyo imeitisha kikao hicho cha dharura ambacho kitafanyika hii leo punde tu baada ya wanachama wa baraza hilo la usalama la Umoja wa Mataifa kuijadili Iraq.
Hapo jana Meja Jenerali Godefroid Niyombare ambaye alikuwa mkuu wa shirika la ujasusi nchini Burundi, alitangaza kuwa utawala wa Rais Pierre Nkurunzinza umepinduliwa na jeshi kutoka madarakani kwa kukiuka matakwa ya raia.

Mara ya mwwisho alikuwa Tanzania
Wakati wa tangazo hilo la kupinduliwa kwa serikali, Nkurunzinza alikuwa Tanzania kuhudhuria mkutano wa viongozi wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki uliotishwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuujadili mzozo huo wa Burundi.
Waandamanaji wakisherehekea kupinduliwa kwa utawala wa Nkurunziza  Waandamanaji wakisherehekea kupinduliwa kwa utawala wa Nkurunziza
Niyombare aliagiza viwanja vyote vya ndege na mipaka yote ya ardhini ya Burundi kufungwa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito wa dharura kwa pande zote nchini Burundi kuonyesha utulivu na kujizuia kufuatia jaribio la mapinduzi ya serikali dhidi ya Rais Nkurunzinza.

Msemaji wa katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephanie Dujarric amesema Ban amesisitiza haja kwa viongozi wote wa Burundi kudumisha amani na uthabiti katika taifa ambalo limekumbwa na matukio ya ghasia mbaya katika kipindi cha nyuma.

Marekani imewataka waburundi kuweka silaha chini kufuatia ripoti za kupinduliwa kwa serikali ya Nkurunzinza na msemaji wa ikulu ya Rais wa Marekani Josh Ernest amesema nchi yake inafuatilia matukio yanavyojiri Burundi kwa makini na wasiwasi.

Marekani imesema bado inamtambua Nkurunzinza kuwa kiongozi rasmi wa Burundi lakini inamshinikiza kuheshimu katiba ya taifa hilo na mikataba ya amani ilyofikiwa mwaka 2000 kwa kutogombea muhula wa tatu.
 
Marekani inatambua utawala wa Nkurunzinza
Hatma ya Nkurunzinza haijulikani baada ya ofisi ya Rais hapo jana kutangza anarejea nyumbani kutoka mkutano wa viongozi wa Afrika Mashariki nchini Tanzania na alitarajiwa kulihutubia taifa.
Baadhi ya wanajeshi wakisherehekea na raia kupinduliwa kwa serikali Baadhi ya wanajeshi wakisherehekea na raia kupinduliwa kwa serikali

Lakini ndege yake haikuweza kutua mjini Bujumbura baada ya viwanja vya ndege kufungwa. Afisa wa ngazi ya juu wa Uganda ambaye hakutaka kutambuliwa kwasababu haruhusiwa kuongea na vyombo vya habari amesema ndege iliyokuwa ikimbeba Nkurunzinza ilitua katika uwanja wa Entebbe nchini Uganda lakini hakutaka kuthibitisha iwapo yuko nchini humo au alirejea Tanzania.

Kiasi ya watu 20 wameuawa tangu tarehe 25 mwezi uliopita baada ya Nkurunzinza kutangaza kuwania muhula wa tatu madarakani kinyume na katiba ya taifa hilo ambayo inaruhusu mihula miwili tu ya miaka mitano kila mmoja akidai muhula wake wa kwanza alichaguliwa na bunge na wala sio wananchi. Zaidi ya waburundi 50,000 wametorokea nchi jirani kufuatia ghasia za kabla ya uchaguzi unaotarajiwa mwezi ujao.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement