Takriban watu 30 wamepoteza maisha
yao baada ya shambulizi la kigaidi katika kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa
kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom.
Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuaji
wa kujitolea mhanga aliendesha gari lake moja kwa moja hadi kwenye lango kuu la
kituo hicho .
Kituo hicho kipo katika eneo la
Leego, barabara kuu inayounganisha mji mku wa Mogadishu na Baidoa.
Wanamgambo hao wa Al shabaab
wamesema wameteka kituo hicho, lakini wanajeshi wa muungano wa Afrika nchini
humo , AMISON wamekanusha madai hayo.
AMISOM inasema kuwa wanajeshi wake
wanaendelea kukabiliana na wanamgambo hao wa kiislamu.
Kundi la al shabaab limeimarisha
mashambulio ya kigaidi tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa mfungo wa ramadan.
Kituo hicho kinaendeshwa na
wanajeshi kutoka Burundi chini ya mwavuli wa (Amisom).
Kituo hicho kinaendeshwa na
wanajeshi kutoka Burundi chini ya mwavuli wa (Amisom).
Jeshi hilo lina zaidi ya askari
20,000 kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
source BBC
Chapisha Maoni