Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Basir Mramba (kulia), Gray Mgonja (kushoto) na Daniel Yona wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.

HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basir Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona imeahirishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi Julai 3, mwaka huu.

Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 11.7

Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na Hakimu Saul Kinemela ambaye ni mmoja wa hakimu yenye jopo la watu watatu kushindwa kufika mahakamani hapo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jaji John Utamwa leo ni kwamba Hakimu huyo yupo mkoani Dodoma kwa shughuli za kibunge na anatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kati ya kesho na keshokutwa.

Amesema kutokana na hali hiyo hawezi kutoa hukumu ya kesi hiyo hadi jopo hilo litakapokamilika.

 SOURCE: Global Publishers.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement