OFISI ya Makamu wa Rais (OMR) imesema kusambaa kwa mifuko ya
nailoni (plastick) pamoja na suala la
muungano ni mambo ambayo yaliipa changamoto kubwa katika kipindi cha
miaka kumi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais
JakayaKikwete.
Yalibainishwa hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam na
Naibu Katibu Mkuu (OMR) Angelina Madette (pichani) alipozungumza na waandishi wa habari
kuhusu mafanikio na changajmoto walizokumbana nazo katika kipindi hicho.
“Katika kipindi cha
awamu ya nne suala la muungano lilitupa changamoto na kuendelea kuwepo kwa
mifuko ya plastiki isiyokidhi vigezo,” alisema.
Alisema katika kukabiliana na usambaaji wa mifuko hiyo OMR
imekuwa ikiongea na watengenezaji ili watengeneze iliyokuwa na viwango
vinavyohitajika.
“Lakini pia temeandaa kanuni ambazo zinaeleza kwamba lazima
kiwango cha unene wa maikroni 50 pamoja na kuhamasisa matumamizi ya mifuko
mingine kama mbadala,” alisema.
Hivi karibuni akijibu swali Bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira Stephen Masele aliwataka watanzania kuacha kutumia mifuko hiyo katika
kuhifadhi chakula kwani ina madhara.
Masele alikiri kuwa mifuko hiyo inaweza kusababisha madhara
kutokana na kemikali zilizotumika kuitengeneza.
Alisema kemikali hiyo inapoingia katika chakula hugeuka kuwa
sumu na kwamba serikali ilipiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo yenye unene wa
chini ya maikroni 30.
Katika changamoto ya muungano, Madette alisema kuliibuka hoja mbalimbali juu ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar ambapo waligundua kwamba elimu ya kutosha kwa wananchi
inahitajika.
“Kuanzia 2006 hadi 2011 Hoja 15 za Muungano ziliwasilishwa
na kujadiliwa na kamati ya pamoja iliyojumuisha nchi zote mbili, kati ya
hizo hoja kumi zimekamika na kuondolewa katika orodha ya changamoto na sita
zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi,” alisema.
Alisema hoja zilizopatiwa ufumbuzi katika kipindi hicho ni
sheria ya Tume ya Haki za Binadamu kutofanya kazi Zanzibar kutokana na sheria
hiyo kutokuwa ya muungano.
Alisema sheria nyingine ya uvuvi katika ukanda wa Bahari
kuu, nafasi ya Zanzibar kuwasilishwa katika miradi ya maendeleo ya kiuchumi kwa
ajili ya miradi ya kikanda inayotekelezwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Miradi ya Zanzibar iliwasilishwa katika Jumuiya ambayo
imefikia katika hatua mbalimbali ni mradi wa uwanja wa ndege wa Pemba, ujenzi
wa bandari ya Maruhubi, ujenzi wa chelezo na kivuko cha kati ya bandari ya
Zanzibar, Dar es Salaam, Pemba, Tanga na Mombasa pamoja na mgawanyo wa mapato
yatokanayo na misaada kutoka nje ya nchi,” alisema.
Alisema changamoto nyingine ambazo zipo katika hatua ya
kutafutiwa ufumbuzi ni ushirikiano wa Zanzibar na taasisi za kimataifa,
utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia, taarifa ya mapendekezo ya Tume
ya pamojaya fedha, kodi nyinginezo pamoja na usajili wa vyombo vya moto.
Chapisha Maoni