Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Wanachama wa chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini – MOAT na wadau wengine wa habari wameazimia kuishauri serikali kuondoa bungeni muswada wa sheria ya upatikanaji wa habari ili kulinda na kudumisha amani, utulivu na demokrasia.


Maazimio hayo yamefikiwa jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa Wanachama wa  MOAT na wadau wengine wa habari, baada ya kupata ufafanuzi wa kina kuhusu muswada wa sheria hiyo kutoka kwa mwanasheria mwandamizi Dr Damas Ndumbaro, na baadaye wajumbe kuujadili  na wazohatimaye kuafiki wazo lililotolewa na Mmiliki wa New Habari Corporation Bw. Rostam Aziz.
 
Mapema Mwenyekiti wa MOAT Dr Reginald Mengi alitahadharisha kuwa hakuna mtu binafsi atakayeweza kuendesha vyombo vya habari iwapo muswada huo utapitishwa kuwa sheria bila ya kufanyiwa marekebisho.
Aidha Dr Mengi pia ameshangazwa na udharura wa kutungwa kwa sheria hiyo wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu, na kusisitiza kuwa amani na utulivu unaweza kupotea na  uchaguzi hauwezi kuwa huru iwapo vyombo vya habari vinanyimwa uhuru wa kupata habari na kuutangazia umma.
Akichanganua kuhusu utata  wa muswada huo Mwanasheria Dr Damas Ndumbaro na Mwandishi wa Habari wa the Citizen wamesema muswada huo pamoja na mambo mengine, unamtaka mwandishi wa habari anayetafuta habari kupeleka maombi rasmi yatakayojibiwa katika kipindi cha siku 30, na inapoteza ajira kwa waandishi wa habari.
 SOURCE: ITV

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement