Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
 christy
Christy Sims ni mwanadada ambaye maisha yake yalibadilika ghafla baada ya aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu kumuachia majeraha ambayo hatokuja kuyasahau maishani.


Akiwa na miaka 40 Christy amelazimika kuishi na makovu baada ya kumwagiwa tindikali  na ex-boyfriend wake kwa sababu tu ya wivu wa mapenzi.

Christy alikumbana na mkasa huo baada ya ex- boyfriend huyo kumhisi kuwa anatembea na mtu mwingine.

christy2Christy Sims kabla ya tukio la kumwagiwa tindikali.
 
Haya yote yalitokea weekend moja ya mwaka 2013 nyumbani kwa mpenzi wake ambaye aliamua kumwagia dada huyu tindikali usoni, kifuani na mikononi kitendo kilichosukumwa na hasira kali za wivu.


Christy alipiga kelele nyingi na kuomba msaada lakini boyfriend wake aliamua kumuacha aungue mpaka watu wa huduma ya kwanza walipofika na kushangazwa kwa nini boyfriend huyo hakuchukua hatua za  kumpatia girlfriend wake huduma ya kwanza.

christy4Christy Sims sasa hivi analazimika kuvaa miwani ya jua kila muda kulinda macho yake yasipigwe na jua la kumuumiza.  

Jamaa alijitetea na kusema ilikuwa ni bahati mbaya lakini Mahakama imeona kuwa mwanaume huyo ana makosa 3, shambulio la kudhuru mwili, na makosa mengine mawili ambayo kwa yote atatumikia kifungo  miaka 60, miaka 20 kwa kila kosa

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement