Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


 
Malik Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini kenya ambako ndiko kilipotokea kizazi chake. 

katika ziara yake hiyo mambo mengi yameibuka hata hivyo hapa nitakuambia kituko cha ndugu yake mmoja.

Habari juu ya ndugu yake huyo imeibuliwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii tangu Rais Obama alipotua nchini humo.

habari hiyo imekuwa ikigusia uhusiano wake na nduguye huyo wa kambo.

Malik Obama ni kaka yake wa kambo na Rais Obama, inaelezwa kuwa mwenendo wa maisha yake unatiliwa shaka kwa sababu si mwaminifu kutokana na  sifa mbalimbali ambazo zimetokana na matukio aliyoyafanya katika familia na jamii yake inayomzunguka.
Malik anahusishwa na kutumia jina la Barack Obama kujinufaisha mwenyewe.

Haijulikani kama sababu hiyo ndiyo iliyosababisha kutoonekana katika chakula cha jioni ambapo Obama  alishiriki pamoja na ndugu zake wengine, akiwamo bibi yake wa kambo, mama sara na dada yake Dk Ouma Obama.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement