Mgombea wa kiti cha urais kupitia
chama cha mapinduzi CCM Dr.John Pombe Magufuli amewataka watanzania
kutofanya kile kinachoitwa maamuzi magumu kama libya ilivyofanya kwa
kumuondoa madarakani rais wa nchi hiyo Muamary Ghadaffi na hii leo
wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao.
Amesema wafanye mabadiliko kama china ilivyofanya katika chama cha Kikomunist cha kufanya mabadiliko ndani ya chama na hivyo na hii leo china imekuwa miongoni Mwa nchi ya kwanza kiuchumi duniani.
Amesema wafanye mabadiliko kama china ilivyofanya katika chama cha Kikomunist cha kufanya mabadiliko ndani ya chama na hivyo na hii leo china imekuwa miongoni Mwa nchi ya kwanza kiuchumi duniani.
Baada ya ufafanuzi huo kuhusu habari ambazo simesambazwa katika
mitandao ya kijamii Dr.Magufuli ambaye amepewa na wananchi jina la mzee
wa kazi akaanza ziara yake ya kusaka ridhaa ya watanzania kiongoza
Tanzania mkoani Njombe ambapo amewataka watanzania kupuuza kile
kinachoitwa mabadiliko kwa kuwa hata Libya ilifanya mabadiliko ya
kukurupuka kutokana na utamu wa lugha za wapinzani wake na hii leo
wananchi wa Libya wanahangaika na kuwataka kumpa fursa ya urais ili
afanye mabadiliko ya kimfumo na kiuchumi taifa lisonge mbele
kimaendeleo.
Aidha Dr.Magufuli akizungumza kwa sauti ya kumaanisha kwa dhati
kile anachokisema amewataka watanzania kumwamini kumpa ridhaa ya kuwa
rais na kwamba Tanzania itaendeshwa bila ya ubaguzi na maendeleo ya
kweli yataonekana.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa Dr.Harrison Mwakyembe
amewaeleza watanzania kuwa Tanzania haitaki viongozi wa maamuzi magumu
na badala yake inamtaka kiongozi mwadilifu atakayesimamia rasilimali za
taifa kwa usawa na haki bila uonevu na ambao wanapaswa kuaminiwa na
wakipewa madaraka hawatadokoa kwa manufaa yao rasilimali za taifa.
Kutokana na kile kinachooneka kuwa sera na kampeni za kistaarabu
zinazofanywa na Dr.Magufuli baadhi ya wananchi waliokuwa katika vyama
vya upinzani wamerejesha kadi zao na kujiunga na CCM kwa kile walichodai
ni kuchoshwa kutumika kama ngazi na viongozi wa CHADEMA.
Jumapili ya August 30 ziara za Dr.Magufuli kusaka ridhaa ya watanzania kuiongoza Tanzania itaendelea mkoani Ruvuma.
Chapisha Maoni