Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

 
mkurugenzi wa Ne, Kailima
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imevitaka vyama vya siasa kuzingatia ratiba ya kampeni ya uchaguzi wa rais kwa kufanya mikutano kwa tarehe, sehemu na mahala kwa mujibu wa ratiba.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na NEC, vyama vyote vya siasa vinatakiwa vizingatie ratiba ya kampeni ya uchaguzi wa rais na viache kufanya mikusanyiko ya aina yoyote ambayo haipo katika ratiba ya kampeni hizo.

Chama kitakachokiuka maelekezo hayo kitakuwa kimekiuka kipengele cha maadili ambacho kinaelekeza kuwa ni wajibu wa vyama vya siasa na wagombea kuheshimu na kutekeleza sheria za uchaguzi, kanuni za uchaguzi, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi pamoja na sheria zingine za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement