Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
 http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/tma.jpg
TAARIFA ZISIZO ZA KWELI ZA UWEPO WA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI KATIKA MAENEO YA DAR ES SALAAM, PWANI, TANGA, UNGUJA NA MTWARA
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawatahadharisha wananchi kuhusu taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya Kijamii inayohusu uwepo wa upepo mkali utakao vuma kwa kasi ya km 123.7 kwa saa na mvua kubwa kwa siku ya tarehe 29/08/2015 kuanzia saa 7 mchana.

Taarifa hii si ya kweli na kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) haijatoa TAHADHARI hiyo.

Utabiri sahihi wa kesho tarehe 29/08/2015 katika maeneo hayo ni kama ifuatavyo: Mvua nyepesi zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo hayo( Dar es Salaam, Pwani,Morogoro, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba).

Upepo unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya wastani wa kilometa 30 kwa saa katika  pwani ya kaskazini( Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba) na kwa kasi ya kilometa 20 kwa saa katika pwani ya kusini(Mtwara).

Aidha, Mamlaka inapenda kuujulisha umma kuwa ina utaratibu maalumu wa kutoa tahadhari kwa kutumia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii





http://meteotz1950.blogspot.com/ 

na tovuti yao ya


hivyo basi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa wito kwa umma kuacha kutoa na kusambaza taarifa za kupotosha katika mitandao ya kijamii.

Imetolewa na:
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement