Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Samia akihutubia katika moja ya mikutano yake

TANGA

MGOMBEA Mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameonya watu waliojipanga kufanya fujo siku ya uchaguzi na kusema bado hajazaliwa mwanamume wa kuisumubua serikali.

Samia alisema hayo jijini hapa wakati akihutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Usagara na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga pamoja na Mgombea Ubunge Jimbo la Bumbuli, Januari Makamba

Samia alisema zipo taarifa zinazosambaa kwamba watu wamejipanga kuwazuia kinamama wasijitokeze kwenye vituo vya kupigia kura na kusisitiza kinamama wajitokeze kwa wingi kupiga kura.

“Jitokezeni mkapige kura ulinzi upo kapigeni kura mkimaliza rudini nyumbani mkasikilize matokeo mwanamume wa kuivimbia misuli serikali bado hajazaliwa” alisema Samia.

Awali Samia aliwahakikishia kinamama wa Tanga Mjini kuwa serikali ya awamu ya tano itahakikishia inalipatia ufumbuzi wa haraka tatizo la maji katika mji huo ili yafikie karibu na makazi yao.

Aidha alisema serikali itaifufua reli ya Tanga, Arusha hadi Musoma kama ilivyoainishwa kwenye ilani ya chama pamoja na kuendelea na kazi ya kuipanua bandari ya Tanga ili kuifanya ipokee mizigo mingi

Pamoja na mambo mengine, mgombea huyo alisema anasikitishwa na tatizo la viwanda vilivyokufa katika jijini humo na kuahidi serikali ijayo itavifufua viwanda vyote vilivyokufa na kuzalisha ajira nyingi kwa vijana.

“Tunatarajia asilimia 40 ya ajira itokane na viwanda na watakaopewa kipaumbele katika ajira ni vijana ili tuondokane na tatizo la vijana wetu kukaa vijiweni,” alisema.

Awali, Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwani serikali na vyombo vya dola vimejipanga ambapo pia alimhakikisha mgombea Mwenza kuwa Magufuli atapata kura zote za ndiyo katika uchaguzi huo.

Surce: MTANZANIA

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement