Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


 
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kutumia vibaya mitandao ya kijamii kufanya uhalifu wa  kutengeneza habari za uongo na uzushi dhidi ya viongozi au watu maarufu.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova amewaeleza waandishi wa habari jijini humo jana kuwa watu hao wamekuwa wakitumia vibaya majina ya watu maarufu hasa wanasiasa.

Aliwataja majina ya wanasiasa hao kuwa ni mgombea ubunge Jimbo la Kibamba, John Mnyika na mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa na baadhi ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na  usalama.

Watuhumiwa hao ni Joel Lumbay (32), Omar Suleiman wote wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Michael Nickson (32) mkazi wa Tegeta, Patrick Natala  na Maxmillian Msacky wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Alisema wamekuwa wakituma jumbe mbalimbali  wakionesha viongozi hao walikuwa wanajadili jambo fulani dhidi ya kundi au chama  kingine cha siasa kwenye mitandao.

“Wana tabia ya kutengeneza ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa lugha iliyozoeleka kama ‘kuchati,’  lakini mawasiliano hayo hayapo… yanakuwa yametengenezwa ili kutimiza malengo yao. Jambo hili ni kosa la jinai na linaweza kuchochea chuki  katika makundi ya watu,” alisema Kova.

Alisema jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wenye tania hizo wakishirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

“Kiongozi  au mtu yeyote atakayeona  ameathirika na mbinu  chafu za kihalifu  asisite kutoa taarifa kwa vyombo  vya dola ili hatua za kisheria zichukuliwe mara moja,” alisema.

Chanzo, MTANZANIA

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement