Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


 

WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) imekanusha uvumi ulioenea juu afya ya Mkuu wa Majeshi ya Usalama na Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange (Pichani), ambao unadai kuwa alinusulika kifo, kwa kile kilichodaiwa kuwekewa sumu kwenye chakula.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na katibu mkuu wa Wizara ya ulinzi na (JKT) Job Masima, ilisema kuwa, uvumi huo ulienda mbali zaidi  baada ya kudai kuwa  mkuu huyo wa majeshi alilazimika kulazwa katika hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Nairobi, nchini Kenya. 

Huku pia ikidaiwa kuwa mkuu huyo amepelekwa nchini India kwa matibabu, jambo ambalo lilikanushwa na kusema kuwa ni uongo wenye kutaka kuleta hofu ya usalama wa watanzania.  

“Taarifa hizo ni za uongo wenye kila dalili ya kutengenezwa kwa lengo la kuwatia hofu watanzania juu ya usalama wa kiongozi huyu wa juu wa majeshi yetu.

“Ukweli ni kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, ni bukheri wa afya na hayupo nchini Kenya wala India kama ilivyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari,” alisema Masima.

Alisema wananchi hawapaswi kuwa na hofu yeyote, kwani taarifa hizo ni uzushi mtupu na kwamba Mkuu huyo aliondoka nchini Septemba 22, mwaka huu kuelekea Rome, Italia kwa ziara ya kikazi.

“Jenerali Mwamunyange, aliondoka nchini Septemba 22, mwaka huu, saa 10.45 jioni kwa ndege ya shirika la ndege la Emirates kuelekea Rome, Italia kwa ziara ya kikazi, kufuatia mwaliko wa Mkuu wa Majeshi  nchi hiyo, Jenerali Claudio Graziano,” alisema Masima.

Alisema wanapenda kuwahakikishia wananchi kuwa Jenerali Mwamunyange, pamoja na ujumbe wake wanaendelea na ziara hiyo kama ilivyopangwa na amesikitishwa na uvumi huo, na kwamba Wizara ya Ulinzi imesikitishwa na uvumi huo. 

“Wizara ya Ulinzi ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), imesikitishwa na tabia hii ya uzushi inayopingana na weledi na kanuni za uandishi katika tasnia ya habari. Ni dhahiri tabia hii inaidhalilisha tasnia ya habari na wanahabari wanaozingatia weledi nchini.,” alisema Masima.

alikemea kuenezwa kwa taarifa za aina hiyo zisizokuwa na tija kwa taifa na zilizolenga kuwasumbua ndugu, jamaa, marafiki na watumishi wenye mapenzi ya dhati na Jenerali Mwamunyange, huku akiwataka wanahabari kutozitumia vibaya taaluma yao.

“Tunawaasa, wanahabari kutozitumia vibaya kalamu zao na uhuru walionao kwa namna yoyote isiyokuwa na tija kwa taifa letu. Aidha, Wizara na Taasisi zake wakati wote zimekuwa tayari kuthibitisha jambo lolote au kutoa ufafanuzi pale unapohitajika,” alisema.

Alisisitiza kuwa ni kitendo cha kustaajabisha kuona walioanzisha uzushi huo na kuueneza hawakuwa tayari kuomba uthibitisho wa namna yoyote, jambo linalotia shaka juu ya nia ya mtu au kikundi kilichoanzisha uvumi huo.  

Alisema Wizara ya ulinzi na Taasisi zake zitaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa wanahabari wenye nia ya dhati ya kujenga na kuiletea sifa tasnia ya habari kwa kuzingatia weledi na kwamba uhuru wa vyombo vya habari uwe ni uhuru wenye kuzingatia wajibu uliobainishwa katika maadili na kanuni za tasnia hiyo.

Pia aliwataka walioanzisha na kueneza uvumi huo kumuomba radhi Mkuu huyo kama ishara ya ustaarabu, na kutambua kuteleza kwao na kwamba kutofanya hivyo itatofasirika kuwa ni kukiri  kueneza uzushi huo na haikuwa kuteleza, bali ilikusudiwa kwa dhamira fulani, na hivyo kushawishi hatua zaidi kuchukuliwa.

“Jeshi na Wizara zitaendelea kushirikiana na mamlaka husika kuwabaini watu waliohusika kuutumia vibaya uhuru wa habari na hivyo kuupotosha umma na kuleta usumbufu kwa familia ya jenerali mwamunyange, Jeshi na Taifa kwa ujumla,” alisema Masima.

Chanzo: MTANZANIA

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement