UGONJWA wa malaria unaweza kuisha
nchini iwapo serikali itasimamia kwa dhati sera na mikakati yake inayoipanga ikiwa
ni pamoja na kudhibiti vitendo vya rushwa katika sekta ya afya.
kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es
Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Phatholog wa Chuo cha Agakhan, Profesa Zul wakati wa uzinduzi wa
dawa mpya ya kutibu malaria ijulikanayo kama Coartem 80/480.
“Takwimu zinaonesha malaria imepungua
kwa asilimia 60 Tanzania lakini nchi ya Sirlanka imefanikiwa kuimaliza kabisa.
Tatizo nililogundua ni kwamba kuna changamoto katika usimamizi wa utekelezaji
wa sera na mikakati inayopangwa na serikali katika kumaliza tatizo.
“Hivyo ni vizuri serikali ya awamu ya
tano chini ya Rais Dk. John Magufuli ambayo inaongozwa na kauli mbiu yake ya
Hapa kazi tu, kuzifanyia kazi changamoto hizo.
Alisema ingawa chanjo ya malaria ambayo
bado ipo katika utafiti ina uwezo wa kuzuia malaria kwa asilimia 30 bado
jitihada zinahitajika katika kupambana na ugonjwa huo.
Naye Msajili wa Baraza la Famasia
nchini, Elizabeth Shekalaghe alisema kwamba ili kuendeleza mapambano
dhidi ya ugonjwa wa malaria jamii inapaswa kuelimsishwa juu ya matumizi sahihi
ya dawa.
Chapisha Maoni