Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Balozi Juma Mwapachu
Mpambe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Balozi Juma Mwapachu ameondolewa katika nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mwapachu ameondolewa katika nafasi hiyo kufuatia kumaliza muda wake ambapo Balozi Dk. Agustine Mahiga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti Mpya.
Balozi Mwapachu (kulia) siku alipokabidhi kadi yake ya uanachama wa CCM kwa Katibu wa Siasa na Uenezi CCM, mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba.

Hayo yamebainishwa na  Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula alitoa alipozungumza na wandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na mahafari ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika Novemba 26 na 27 mwaka huu.

Akizumzungumzia Mwenyekiti mpya Prof Idris amesema  amesema kuwa Balozi Mahiga ni mzoefu katika utumishi na amefanya kazi nzuri nje na ndani ya nchi huku akiwa na matumaini makubwa kwamba ataliongoza baraza hilo bila hofu yeyote.

Kwa  upande mwingine  amesema Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amemuongezea muda wa miezi sita, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Shaban Mlacha ambaye alipaswa amalize muda wake Desemba 30, mwaka huu. 

Siku kadhaa zilizopita Balozi Juma Mwapachu alitangaza  kuachana na chama Mapinduzi na kutimkia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa madai  ya kutoridhishwa na mwanasiasa Edward Lowassa kukatwa katika mchakato wa urais ndani ya chama Chama Mapinduzi.

Chanzo, hivi sasa.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement