Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

DAR ES SALAAM
WATU 9,906 wameugua ugonjwa wa kipindupindu katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi miwili, Katika kipindi hicho, jumla ya watu 149 wamefariki duniani kutokana na kuugua ugonjwa huo. 
 
Takwimu hizo zimetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donald Mmbando (pichani), katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Mkutano huo ulikuwa mahususi kwa ajili ya kuhimiza utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi siku ya maadhimisho ya Uhuru, Desemba 9, mwaka huu.

“Tatizo ni kubwa, lakini tunaweza kulizuia kwa kufanya usafi wa mazingira yetu kwa sababu chanzo kikuu cha ugonjwa huu ni uchafu,” alisema Dk. Mmbando.

Aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na maofisa wa afya kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa agizo hilo na kulifanya suala la usafishaji mazingira kuwa endelevu.
“Ninawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli ya usafi na utahusu maeneo ya Makazi, ofisi na biashara mbalimbali,” alisema Dk. Mmbando.
Aidha, aliwataka watendaji wa serikali wa ngazi zote kudhibiti utupaji taka holela kwa kusimamia ukusanyaji, usafirishaji na uteketezaji salama wa taka pamoja na kusimamia sheria
ya utunzaji wa mazingira.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement