Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
IMG_0910
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Dk. Hamis Kigwangwala akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Lawrence Museru
SERIKALI imenunua mashine mpya ya CT-Scan kwa ajili ya kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). 

Mashine hiyo yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 1.7 (takribani Sh bilioni 3.6) imeelezwa kwamba ni yenye uwezo wa hali ya juu.

Ununuzi wa mashine hiyo, umefanyika baada ya agizo la Rais John Magufuli alilolitoa hivi karibuni akiutaka uongozi wa MNH kuboresha huduma zake kwa kuhakikisha vifaa tiba na dawa vinapatikana ili Watanzania wapate huduma bora ya matibabu.


Ununuzi wa mashine hiyo ulielezwa jana na Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare, wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kingwangalla alipofanya ziara katika hospitali hiyo kubwa zaidi nchini.Dk Kigwangallah pia alitembelea Idara ya Magonjwa ya Dharura, Idara ya Mionzi na sehemu mpya ya wagonjwa waliopo chini ya uangalizi maalumu (ICU). 


Dk Lwakatare alisema kwamba CT-Scan hiyo mpya imetengenezwa na kampuni ya Siemens na kwamba imefungwa siku mbili zilizopita

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement