ASILIMIA 80 ya watu wenye ulemavu wa ngozi hufariki dunia kila mwaka nchini kwa kukosa matibabu dhidi ya tatizo la saratani ya ngozi.
Akizungumza na MATUKIO NA MAISHA hivi karibuni jijini Dar es
Salaam kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Saratani duniani Ofisa Mahusiano wa Chama
cha Albino Tanzania (TAS), Josephat Tona alisema hiyo ni kwa sababu huchelewa
kufika katika vituo vya afya.
“Umri wa kuishi wa albino ni miaka 35 na 40 tofauti na watu
wengine ambao hufika hadi kati ya miaka 50 hadi 70. Asilimia 80 wanafariki kwa
sababu ya kuugua saratani ya ngozi ambayo kwa mujibu wa watalaamu inasababishwa
na miale ya jua,” alisema.
Alisema ili kujikinga dhidi ya saratani hiyo huhitaji
mafuta maalumu ya kupaka kwenye ngozi hata hivyo hushindwa kumudu gharama ya
kuyanunua mafuta hayo.
“Naiomba serikali itenge bajeti itakayowezesha Albino kupata
huduma za afya zilizo bora, itusaidie pia kupata mafuta ya kuzuia mionzi ya jua
ambayo ni ghali na mara nyingi huwa yanatoka nchi za Ulaya, nakumbuka mara ya
mwisho ilikuwa 2013 ambapo tulipatiwa jumla ya ‘tube’ 4000 za mafuta za kugawa
nchi nzima ambayo kimsingi hazitoshi,” alisema.
Chapisha Maoni