Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


 
MKAZI wa Mabibo jijini Dar es Salaam, Abraham Warioba (50), amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh milioni 39 baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki Digidigi 20 huku vibali vyake vikiwa vimeisha muda jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan baada ya kujilidhisha na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na mashahidi wanne wa upande wa mashataka ambao ni Serikali.

“Mahakama inamtia hatiani mtuhumiwa kwa kumiliki Digidigi 20 ambazo ni nyara za serikali kwa vibali vilivyoisha muda wake jambo ambalo nikinyume cha sheria, hivyo atatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani au kulipa faini Sh. Milioni 39, adhabu hii itaanza mara tu baada ya kukamatwa.

“Kwani alipo ni rahisi tu kuweza kukamatwa kwakuwa kila kitu kipo cha kumfanya akamatwe, hivyo mahakama inatoa amri akamatwe ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia za kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria,” alisema Hakimu Hassan.

Warioba ambaye pia ni mfanyabiashara aliruka dhamana wakati shahidi wa tatu akiwasisha ushahidi wake hivyo ataanza kutumikia adhabu hiyo mara baada ya kukamatwa.

Kesi hiyo ilikuwa na Mawakili wawili wa serikali ambao ni Florida Wenceslaus na Chesense Gavyole, ambao waliiambia mahakama hiyo kuwa hakukuwa na kumbukumbu za  makosa ya nyuma dhidi ya mshtakiwa na hivyo kuiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia kama hiyo ya kumiliki nyara za serikali pasi kuwa na vibali halali jambo linaloiingizia hasara taifa.

Katika hati ya mashtaka, Warioba anadaiwa Januari 17 mwaka 2011 eneo la Pugu Kigogo Fresh, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, alikutwa akimiliki Digidigi 20 wenye thamani ya Sh milioni 3.9 ambao ni nyara za serikali huku vibali vyake vya kumiliki wanyama hao vikiwa vimeisha muda wake jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement