Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
 
Ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.

Ndege hiyo ya A320 ilianguka saa tano asubuhi katika Kusini mwa Milima ya Alps.

Viongozi wa Ujerumani na Ufaransa wanaendelea kushauriana kuhusiana na mkasa huo unaowakabilia macho.

Ndege hiyo ya Ujerumani ilianguka katika eneo lisilo na mijengo ambalo halifikiki kwa urahisi nchini Ufaransa Kusini mwa Milima ya Alps.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaja ajali hiyo kama mkasa na amesema kuwa uwezekano wa kuwapata watu wakiwa hai ni mgumu.

Hali ya hewa katika eneo hilo ilitajwa kuwa nzuri na kituo maalumu cha kukabiliana na mikasa kimetengwa kukabiliana na mkasa huo.

Waziri wa Maswala ya ndani ya nchi uko njiani kuelekea mahali pa ajali hiyo.

Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe wa kuwa hatarini kabla ya mawasiliano yake kutoweka .



Rubani msaidizi, Andreas Lubitz, aliangusha makusudi ndege hiyo kwenye milima ya Alps

Picha za ajali zanaswa

Gazeti moja nchini Ujerumani na jarida la Ufaransa yameripoti kuwa yameona picha za video zilizopigwa kwa simu zinazoonyesha dakika za mwisho ndani ya ndege ya Germanwings iliyoanguka katika milima ya Alps wiki iliyopita.

Picha hizo za video zinadaiwa kuwa zilipatikana kwenye programu ya kuhifadhi kumbukumbu yaani memory-card iliyopatikana eneo la tukio. 

Katika picha hizo abiria ndani ya ndege hiyo wanaonekana wakipiga kelele huku sauti ya rubani na jitihada za kutaka kufungua mlango ili aingie kuokoa ndege hizo zikisikika. 

Rubani msaidizi wa ndege hiyo, Andreas Lubitz,anayeaminika kuwa ndiye aliyesababisha ajali hiyo alikuwa ndani ya chumba cha ndege huku akiqwa amefunga mlango mwenzake asiingie.
 
 Moja ya ndege zinazomilikiwa na shirika hilo

Wachunguzi wa ajali hiyo watoa neno

Wachunguzi kutoka Ufaransa, wamependekeza sheria kali inayozuia madaktari kufichua siri za marubani wagonjwa iondolewe.

Wanasema iwapo sheria hiyo isingelikuwepo , ajali iliyosababishwa na rubani mwenza aliyekuwa amezongwa na mawazo isingelitokea.

Wachunguzi hao pia wanasema haifai kuwa marubani wanaruhusiwa wenyewe kujitathmini hali yao ya kiafya.

Wachunguzi hao walitoa mapendekezo hayo katika ripoti yao ya mwisho kuhusiana na ile ajali mbaya ya ndege ya shirika la ndege la Germanwings, iliyoangushwa makusudi na rubani mwenza katika milima ya Alps.

Wanatarajiwa kutoa baadhi ya mapendekezo waliyopata kutoka kwa data ya kifaa cha kurekodi sauti ya ndege hiyo.

Ripoti hiyo ni pamoja na hali ya kiakili ya rubani huyo na usalama wa chumba cha rubani pamoja na hali ya kiafya ya marubani.

Abiria wote 150 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, iliyokuwa ikitokea Barcelona kuelekea Dusseldorf Nchini Ujerumani, waliangamia.

Rubani msaidizi, Andreas Lubitz, aliangusha makusudi ndege hiyo kwenye milima ya Alps.

Ilifahamika baadaye kuwa Lubitz alikuwa na msongo wa mawazo, baada ya kukosana na mpenziwe wa kike, lakini sheria za kisiri za Ujerumani zinazuia madaktari kutoa siri za ugonjwa wa wateja kwa waajiri.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement