Mbunge wa Jimbo la Mikumi na msanii wa bongo fleva, Joseph Haule maarufu kama Prof Jay amesema kuwa yeye ni mwanamuziki na ataendelea kufanya muziki mpaka siku atakapotoweka duniani.
Prof Jay amefunguka hayo baada ya
Babutale kutaka kufahamu ni lini msanii huyo ataachia kazi nyingine
kwani toka amekuwa mbunge wa jimbo la Mikumi amekuwa kimya kwenye sanaa
na kusema kuwa amekumbuka mashairi ya msanii huyo, ndipo hapo Prof Jay
alipoweka sawa kuwa kwa sasa yeye ni mbunge wa Mikumi hivyo ana kazi
kubwa ya kuwatumikia wana Mikumi na kusema kwamba jambo hilo pia
haliwezi kufanya ashindwe hata kwa uchache kuendelea kufanya muziki.
“Nakushukuru sana Babutale kwa kuendelea
kuniamini. Pia nimepata salaam nyingi za kunimiss kwenye game kutoka kwa
mashabiki wangu wengi sana kutoka kona mbalimbali za dunia hii.
Ni
kweli kabisa kwamba kwa sasa nina majukumu makubwa sana ya kuwatumikia
wananchi wenzangu wa jimbo la Mikumi lakini hilo halisababishi mimi
kushindwa hata kwa uchache kuendelea kufanya muziki na kuwatendea haki
mashabiki wangu wa ukweli walionibeba tangu siku ya kwanza mpaka sasa
wanaendelea kuwa pamoja sana na mimi, ikumbukwe mimi ni mwanamuziki na
nitaendelea kuwa mwanamuziki mpaka nione kibao kimeandikwa hakuna
muziki”. Alisema Prof Jay
Mbali na hilo Prof Jay amefunguka na
kusema muziki kwake ndiyo ulifungua njia katika maisha yake na leo
kumfanya kupata heshima kubwa kwa watanzania hususani kwa watu wa Mikumi
kama mbunge wao, kutokana muziki ambao alikuwa akifanya.
“Muziki umenilea, muziki umeendesha
maisha yangu na familia yangu, muziki ndio ulionipa heshima kubwa sana
ulimwenguni, bila muziki leo nisingekuwa mbunge wa Mikumi.
Nawaahidi
mashabiki wangu wote mliokuwa mnaniuliza mara kwa mara kama nimeacha
kufanya muziki kuwa nitaendelea kufanya muziki till i die, maana hiki ni
kipaji cha hali ya juu nilichopewa na Mungu kwa makusudi na kwa
Upendeleo mkubwa na sio kwa bahati mbaya.
Nimewasikia na muda sio mrefu
nitawatendea haki, ahsanteni sana kwa kuniamini nawapenda sana, huu ni
mgodi unaotembea” Prof Jay
Chapisha Maoni