WAJASIRIAMALI zaidi ya 50 Visiwani Zanzibar wamepatiwa mafunzo maalumu na benki ya Afrika
Tanzania ili kuwajengea uwezo wa kibiashara na kiuchumi.
Mafunzo hayo yalitolewa mwishoni mwa wiki visiwani humo na ikiwa sehemu ya
uzinduzi wa Benki ya Afrika Tanzania tawi la Zanzibar katika Kuhakikisha utekelezaji wa mpango wa ukuzaji
wa mtandao wake nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo,
Balozi Mwanaidi Sinare Maajar katika uzinduzi huo alisema imewekeza katika kustawisha uchumi wa Tanzania
kwa kueneza matawi yake kwenye maeneo
mbalimbali ya Tanzania katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro,
Mwanza, Mbeya, Morogoro, Shinyanga, na Mtwara.
Mwanaidi aliongeza kuwa tawi hilo lililozindiliwa
Visiwani humo ni la 22 kwa Tanzania ambapo mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka
2015, BOA ilifikisha faida ya bilioni 7 za kitanzania kutokana huduma bora
zinazoendelea kutolewa sehemu mbalimbali nchini.
Alisema kuwa wamechagua Zanzibar kutokana na uwezo
wake mkubwa Hasa katika kilimo cha viungo, uvuvi, biashara na utalii,ambapo
huduma za kukidhi mahitaji kwa wananchi zitatolewa kwa ubora unaotakiwa.
Naye waziri
wa fedha wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Omar Yussuf Mzee, aliyekuwa mgeni
rasmi katika ufunguzi huo alisema kuwa Serikali inatambua kwamba maendeleo ya
kukuza uchumi na kuondoa umaskini hayawezi kufanikiwa bila ya kushilikisha
Sekta binafsi pamoja na sekta ya kibenki.
Chapisha Maoni