RAIS wa Rwanda, Paul Kagame anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi kwenye kongamano la biashara, viwanda na usafirishaji linalotarajiwa
kufanyika Mei 20 mwaka huu Kigali Rwanda.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania, Dk
Kingu Mtemi alisema kuwa, lengo la kongamano hilo ni kutoa fursa za kibiashara
katika sekta mbalimbali ikiwamo, viwnada, nishati na madini, usafirishaji na
kilimo.
Alisema kutokana na hali hiyo, zaidi ya
wafanyabiashara 100 kutoka Tanzania wanatarajiwa kushiriki kwenye kongamano
hilo hali ambayo itaweza kuleta ushirikiano wa karibu na kuongeza uzoefu.
“Tunatarajia kupeleka wafanyabiashara zaidi ya 100
kwenye kongamano hilo ili waweze kupata fursa ya kubadilishana mawazo na
kuongeza masoko katika shughuli zao,”alisema Mtemi.
Aliongeza, hali hiyo itasaidia kukuza uchumi na
kuongeza mapato jambo ambalo linaweza kusaidia kuongezeka kwa ushirikiano wa
karibu baina ya nchi hizo mbili.
Alisema, mpaka sasa, zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa
zinazokwenda nchini Rwanda zinatumia bandari na magari ya Tanzania, jambo
ambalo linaonyesha wazi kuwa, nchi hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kukuza
uchumi.
“Kila mwaka tunapata bidhaa zaidi ya asilimia 800
ambazo zinatoka nchi mbalimbali kwenda Rwanda kupitia bandari ya Tanzania,
lakini pia bidhaa hizo zinasafirishwa na magari yanayotoka kwenye kampuni za
hapa nchini, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa, nchi hiyo inachangia kukuza
uchumi,”alisema.
Alisema, kutokana na hali hiyo, wafanyabiashara hao
wataparta fursa mbalimbali ambazo zitawaongezea kipato na kuleta mahusiano wa
karibu kwa wahusika.
Alisema, mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa, wadau
wa kongamano hilo wanatoa elimu kwa
wananchi na wafanyabiashara kwa ujumla ili waweze kujitokeza na kushiriki
kwenye kongamano hilo kwa ajili ya kuongeza uzoefu.
Chapisha Maoni