Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


 
WANAWAKE wapatao 670 nchini wanafariki dunia kila mwaka kwa tatizo la ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi. Idadi hii ni wale wanaofika kupatiwa matibabu katika Taasisi ya Ocean Road (ORCI).

Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na Dk. Frida Mghemba wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakati alipokuwa akiwasilisha mada katika semina ya siku moja kwa waandishi wa habari iliyolenga kuwajengea uwelewa juu ya masuala ya chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwamo huo wa saratani ya shingo ya kizazi.

“Tatizo hilo husababishwa na kirusi ambacho kitaalam kinajulikana kama Human Papiloma Virus (HPV)  ambacho kipo katika aina zaidi ya 40.  Lakini aina ya 16 na 18 ndio vinatajwa kuwa hatari zaidi kwa kusababisha maambukizi kwa asilimia 70,” alisema.

Alisema hata hivyo huwa si rahisi kumtambua mwanamke aliyeambukizwa virusi hivyo ambavyo huenea kwa njia ya kujamiiana hadi pale atakapochunguzwa kwa kipimo maalumu cha kimaabara.

“Kwa bahati mbaya wanawake wengi hawana mwamko wa kujitokeza kupima afya zao kwa kuchunguzwa iwapo kama wana saratani na mara nyingi hufika hospitalini ugonjwa ukiwa hatua ya tatu na nne ambazo mara nyingi huwa si rahisi kupona ukiwa katika hatua hiyo,” alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Mpoki Ulisubsya alisema ili kukabiliana na hali hiyo serikali imeanza kuwapatia chanjo wasichana ili kuwakinga dhidi ya kirusi hicho cha HPV.

“Mpango huu umeanza kutekelezwa mkoani Kilimanjaro ambapo wasichana wenye umri wa miaka 9 katika wilaya saba za mkoa huo wamepatiwa chanjo lakini lengoletu ni kwamba ifikapo mwaka 2017 tuwe tumepeleka chanjo na kuwapatia wasichana nchi nzima 2017,” alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement