WASANII mahiri wa muziki wa bongo flavor akiwamo
Vanessa Mdee, Navy Kenzo, Weusi, pamoja na kundi la vichekesho la ‘Orginal
Comed’ wamekubali kujitolea kuelimisha jamii juu ya ugonjwa wa sickle cell.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam
na Mwanaharakati wa masuala ya sickle
cell, Uingereza Yasimin Razak alipozungumza na waandishi wa habari.
“Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani
(WHO) Tanzania inashika nafasi ya nne kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa
sickle cell, na wataalamu wanasema ni tatizo linalowapata watu weusi pekee,”
alisema
Alisema hata hivyo jamii haina uwelewa wa kutosha juu
ya ugonjwa huo hivyo amejitolea kushirikiana na wasanii kupeleka elimu.
“Nilikutana na wasanii wengi mwishoni mwa wiki na
hawa ni miongoni mwa wasanii walioonesha nia ya kushiriki katika kampeni ya
kuelimisha jamii ambayo natarajia kuifanya Juni 19, mwaka huu ambayo ni siku ya
Sickle cell duniani,” alisema.
Chapisha Maoni