Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEikOSLhdC__sbh8XYy6Kr5Wxp1Jo2hEY0Vpg8aZAOwPe-0uxzQBxHNAItWHAD7RnlttN-W6OjRP1Wg-9shzPxN0cHCcHoku6mAdlIneo4gphUeL1L0GFInldm-KrypCXAHrmrBpuHkXKic/s1600/chibu1.jpg
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni hiyo, Fred Kazindogo

Kampuni ya Dar Brew ambao ni wazalishaji wakuu wa bia ya asili ya Chibuku imesema bia hiyo maarufu kwa jina la Chibuku super itaanza kuuzwa hadi kwenye maduka makubwa (Super Market) nchi nzima kwa bei ya Sh. 1000.

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni hiyo, Fred Kazindogo alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa chupa yenye muonekano mpya wa Chibuku super yenye ujazo wa milimita 750.

“Chibuku Super itaanza kupatikana nchi nzima katika baa, maduka makubwa ‘super market’ katika maduka ya jumla na rejareja na sehemu zinazouzwa vileo kuanzia leo. Nina imani kubwa wapenzi wa bia yetu wataipokea kwa shangwe na wataitumia ili kuonyesha kuwa wanajali asili yao,” alisema Kazindogo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWgrXGNPXhnu1kVosZbt9Hg5CnjRyOduzdDJvVaGL3Ft-krKHrt6-Ij49Snlz5XXLlu2n2EOcWBrZg5gAgkENeB3C0blbBOR16PHJZW4-vSm-9V490IdO8i-kPSQ7A6LQxjvOe8ePhh9c/s1600/MMG_7227.jpg
Naye Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Oscar Shelukindo (mwenye miwani) alisema mtumiaji atakayenunua kinywaji hicho hatalazimika tena kurudisha chupa mahala aliponunua na kwamba imewekwa katika chupa nzuri ya plastic inayovutia.

“Bia hii imetengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ya kisasa kabisa, hivyo tunawahakikishia watumiaji ubora wa hali ya juu,” alisema.

Shelukindo alisema bia hiyo imetengenezwa kwa kutumia malighafi za nyumbani ikiwemo nafaka ya mtama ulio bora hivyo hakuna sababu kwa watanzania kujivunia kilicho chao na kukumbuka asili yao kwani hii ni bia yao ya asili.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement