Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Godfrey Frank ambaye umri wake haukuweza kupatikana amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu na rafiki yake aliyefahamika kwa jina Hassan Hemed (22).

Mauaji hayo yaliyotokea Mei 16 maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam majira ya saa 2 usiku ambapo inadaiwa mtuhumiwa alimtaka marehemu kumnunulia pombe aina ya kiroba hali iliyosababisha kutoelewana baada ya marehemu kudai kuwa hakuwa na pesa ya kumnunulia.

Taarifa zilizoifikia gazeti hili zilidai kuwa baada ya marehemu kumwambia mtuhumiwa wa mauaji kuwa hakuwa na pesa kwa wakati huo, mtuhumiwa alimtaka kuweka dhamana ya viatu vyake jambo ambayo marehemu hakukubaliana nalo ndipo mtuhumiwa huyo wa mauji  akaamua kumchoma kisu maeneo ya mabegani na kusababisha kupoteza maisha akiwa njiani kuelekea hospitali.

MTANZANIA iliwasiliana na Kamanda wa Polisi Kinondoni, Christopher Fuime ili kuthibitisha tukio hilo alisema walipokea taarifa za mauaji hayo majira ya saa 2 usiku na kwamba mtuhumiwa wa tukio hilo la mauaji alidai kuwa alikuwa anamdai chenji marehemu baada ya kununua sigara.

Alisema kwa mujibu wa taarifa walizopokea, tukio hilo linadaiwa kutokea majira ya saa 2 usiku  maeneo ya Mikocheni A jijini Dar es Salaam na kwamba bado upelelezi unaendelea.

“Ni kweli tumepokea taarifa za tukio hilo la mauaji lakini bado hazijaeleweka vizuri kutokana na mtuhumiwa anaonekana kama mtu asiekuwa na utimamu kichwani na mwenzake waliegombana amefariki,” alisema.                              

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement