picha hii inaonesha sehemu mbalimbali za mwili wa mwanaume
Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
WANAUME ambao korodani zao hazijashuka kwenye
mfuko wake wapo hatarini kwani kuna uwezekano mkubwa wa kugeuka kuwa saratani
zikiwa tumboni.
Korodani ni kiungo muhimu mno katika mwili wa
mwanaume kazi yake kuu ikiwa ni kuzalisha mbegu za kiume pamoja na homoni za
kiume (Testosterone).
Daktari Bingwa wa Mfumo wa Njia ya Mkojo
(Urolojia) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Ryuba Nyamsogoro alisema mapema wiki hii alipozungumza na
MTANZANIA kwenye mahojiano maalumu.
“Kawaida mwanaume ana korodani mbili, moja ikiwa
upande wa kushoto na nyingine upande wake wa kulia.
Huwa zinatengenezwa tumboni na baadae hushuka hadi katika vifuko vyake vilivyoko nje ya mwili wa mwanaume karibu na uume.
Huwa zinatengenezwa tumboni na baadae hushuka hadi katika vifuko vyake vilivyoko nje ya mwili wa mwanaume karibu na uume.
“Huwa zinatengenezwa ndani ya tumbo la mtoto wa
kiume na huanza kushuka kuelekea kwenye vifuko vyake kupitia mrija wake wa
Gubanakulamu mimba ikiwa Katika kipindi cha kati ya mwezi wa sita na saba tangu
ilipotungwa ,” alisema.
Alisema hata hivyo kuna wakati korodani huwa
hazishuki licha ya muda wake wa kushuka kuwa umefika na kwamba hiyo hutokana na matatizo mbalimbali na wapo
wengine ambao hujikuta hazishuki zote mbili ingawa hawa ni wachache,” alisema.
Daktari huyo alisema hakuna dalili zozote ambazo
mjamzito anaweza kuziona na kujua kuwa mtoto aliyembeba tumboni atakuwa na
tatizo hilo siku zijazo.
Chapisha Maoni