Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
WANAWAKE WAANDAMANA WAKIDAI KUKOSA WANAUME WA KUWAPA UJAUZITOWanawake katika jimbo la Ndeiya nchini Kenya walifahamisha kuwa waume zao wanashindwa kuwapa ujauzito kutokana na mwenendo wa unywaji wa pombe haramu ambazo zinaathiri nguvu za kiume.


Katika maandamano ya amani yaliofanyika katika kituo cha biashara cha Thigio, wanawake walioandamana Akhamisi walifahamisha kukerwa na wanaume wanaojihusisha na ulevi kupita kiasi.

Nancy Wangare alifahamisha kuwa katika kijiji
hicho wanawake wachache walioolewa wamevumilia kwa kiasi kikubwa kutokana na upungufu wa nguvu za kiume kwa waume zao kutokana na pombe wanazokunywa.

Mmoja miongoni mwa wanawake walikuwa wakiandamana alifahamisha kuwa iwapo tabia hiyo ya ulevi haitorekebishwa basi itawalazimu kutoka nje ya ndoa zao na bila wao kujua lolote na kuwahudumia watoto wasiokuwa wao.
 
Chanzo: The Choicetz

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement