Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Mwandishi maalum-Geneva
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na W
atoto, Ummy Mwalimu  wakati akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani
unaofanyika nchini Geneva,Uswisi.

Ummy alisema licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga
hatua  katika sekta ya afya kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia  vifo 54 kati ya vizazi hai 1,000 kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000.

Aidha, mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani,
Tanzania imetambuliwa na kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa polio kwa kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa watoto.

“Ninaeleza kwa masikitiko kuhusu tatizo la mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu uliopo nchini Tanzania  ambapo hadi kufikia  tarehe 22 Mei, 2016 idadi ya wagonjwa ilifikia 21,581,kati yao watu 338 wamepoteza maisha, naahidi Serikali kupitia wizara ya afya  itaimarisha  na kuzingatia
kanuni za afya ya mazingira katika kukabiliana na ugonjwa huu”alisema.

Kwa upande wa kutokomeza malaria waziri Ummy alisema Tanzania imeweza
kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu kutoka asilimia 18 hadi 9.5 kwa
Tanzania bara na kwa upande wa Zanzibar  imefanikiwa kupunguza idadi ya  wagonjwa  hadi kufikia asilimia 0.6 .

Katika kuboresha huduma za afya nchini alisema Serikali ya Tanzania
imejipanga na kuhakikisha itaboresha huduma za afya ziweze kumfikia kila
mtanzania  popote alipo, “ili kuweza kufikia malengo haya ni wakati muhimu sasa kuwekeza zaidi katika sekta hii kwa kuongeza uwekezaji katika raslimali fedha,watu pamoja na kuboresha miundombinu ikiwemo utoaji wa huduma za afya nchini”.

Waziri Ummy alisema katika kufikia mafanikio ,wizara ya afya inatarajia
kuwasilisha muswada wa sheria katika bunge la mwezi wa Septemba,2016 wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya kitu ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa mwananchi katika kupata huduma za matibabu wakati wowote anapokuwa na fedha  au kutokuwa na fedha kwa kuwa maradhi hayachagui wakati.

Mkutano mkuu wa mwaka  wa Afya Duniani hufanyika  nchini Geneva –Uswis kila
mwaka mwezi mei ambao huwakutanisha  mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa  Shirika la afya Duniani {WHO} na kuhudhuriwa na wadau, mashirika na taasisi zinazoshiriki katika kutoa huduma za afya Duniani.
 
Tanzania inawakilishwa na waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy mwalimu na Waziri wa
Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Kombo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement