Jengo la JKCI lililoko ndani ya Muhimbili
Na Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam
ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
wamechangia damu katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni hatua ya kuwezesha upasuaji wa watoto wapatao 70 wanaosubiri upasuaji huo.
Akizungumza na mtandao huu hii leo jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi (pichani) amesema wamepata
chupa zaidi ya 20.
“Tunashukuru kwa askari wetu wa JWTZ kuchangia damu,
tuna watoto zaidi ya 70 wanaosubiri kuanza kufanyiwa upasuaji kuanzia Agosti 9
hadi 19, mwaka huu.
“Lakini wakati huo huo tunakabiliwa na uhaba wa damu,
tumepata chupa zipatazo 24 toka kwa wanajeshi wetu na kesho wamesema watakuja
tena, tunaomba watanzania wengine nao waungane nao kuja kuchangia damu ili
tuokoe maisha ya watoto hawa,” amesema.
Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ),Kanali Ngemela Lubinga(aliyesimama) alipokabidhi taarifa kwa mkuu wa mkoa Paul Makonda juu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ ambapo pia alisema watajitolea kuchangia damu.
Amesema JKCI wanatarajia kuwafanyia upasuaji huo kwa kwa
kushirikiana na wataalamu wenzao wa nchini Marekani na Italia.
“Kuna watoto wapatao 500 wanasubiri huduma ya
upasuaji.
Tunaanza na hawa 70 Agosti 9 hadi 19, mwaka huu, tutatumia njia ya
upasuaji pasipo kufungua kifua ambapo
kwa siku tutaweza kuwafanyia watoto 11 hadi 12,” amesema.
Chapisha Maoni