MWANAHABARI nguli nchini Jenerali Ulimwengu ambaye alilazwa katika
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) kwa matibabu ameruhusiwa.
Akizungumza na mtandao huu juzi katika wodi namba H saa chache kabla
ya kutoka kurejea nyumbani kwake, Ulimwengu alisema anamshukuru Mungu afya yake
imeimarika.
Ulimwengu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri wa gazeti la
Raia Mwema alipata ajali ya gari usiku wa Agosti 25, mwaka huu.
Alipata majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake hali ambayo
ilipelekea kulazwa hospitalini hapo ili kupata matibabu.
Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi ajali hiyo
inadaiwa kuwa ilitokea kati ya makutano ya barabara ya Ally Hassan Mwinyi na
Kenyata.
Mvungi alisema Ulimwengu ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya
daktari wake kuridhishwa na maendeleo ya afya yake.
Chapisha Maoni