Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
NA CATHERINE SUNGURA, SIHA

UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha wametakiwa kurekebisha miundombinu yote stahili ya kituo cha afya ikiwemo kutengeneza chumba cha upasuaji pamoja na wodi za kulaza wagonjwa ili kuweza kukidhi hadhi na kuwa hospitali ya wilaya.
 
Hayo yamesemwa jana na Naibu WWaziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi kigwangwalla wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa kituo hicho wa majengo pamoja na kujionea utoaji huduma kwa wakazi wanaoizunguka wilaya hiyo.
 
Dkt. Kigwangwalla alitoa maelekezo hayo baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Onesmo Buswelu kukumbushia ombi lao la awali kwa wizara hiyo ya kutambulika kwa kituo hicho kuwa hospitali ya wilaya ili kurahisisha utoaji wa huduma za afya kwa wakazi wake.
 
Hatahivyo ombi hilo halikukataliwa na Naibu Waziri huyo bali aliwataka kuweza kutekeleza ushauri ule waliopatiwa na wizara yake ya kukidhi vigezo stahili kulingana na miongozo ya upandishwaji wa hospitali ya wilaya
 
"Mkurugenzi tumieni mapato ya ndani ,muweze muweze kutengeneza chumba cha upasuaji pamoja na wodi za kulazwa wagonjwa kwa kutumia majengo hayahaya ya juu hata mkimalizia machache na kuboresha kuliko kusubiri kujenga jingo jipya "
 
Kwa upande wa ukusanyaji na utupaji taka naibu Waziri huyo alimtaka kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya kuzingatiia miongozo na taratibu za ukusanyaji wa taka kwenye vyumba vya kutolea huduma kwa kuzingatia rangi na kuweka alama vifaa vinavyotumika kama ilivyopendekezwa na wizara uli kuweza kuwakinga watoa huduma na wagonjwa na magonjwa ambukizi yatokanayo na taka.
 
"Mkuu wa Wilaya,hawa wote hakuna asiyejua miongozo ya utunzaji taka kwenye vyombo vya kutolea huduma,ndoo hizi zinauzwa kiasi gani,lazima mtekeleze miongozo hii ili muweke kuwakinga watoa huduma wenu"alisema Dkt. kigwangwalla

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement