NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM
IDADI kubwa ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi
18 hasa wa kike wanafanyiwa vitendo vya ngono katika ngoma za usiku ‘vigodoro’.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara hiyo, Sihaba
Nkinga alisema hayo juzi alipozungumza na MTANZANIA, saa chache baada ya
kumalizika kwa semina ya siku moja ya waandishi wa habari kuhusu masuala ya
ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Nkinga alisema watoto wengi waliohojiwa na maofisa wa
Wizara hiyo walikiri kufanyiwa vitendo hivyo kwenye vigodoro hali
iliyowapelekea wengine kupata ujauzito wakiwa na umri mdogo.
“Hali ya ukatili wa kijinsia nchini ni mbaya, wanawake
wengi na watoto wanafanyiuwa ukatili, lakini mwaka 2009 tulifanya utafiti na matokeo
hayo yalitoka mwaka 2011, watoto wengi waliohojiwa walikiri kufanyiwa vitendo
vya ngono kwenye vigodoro.
“Tuligundua pia zipo baadhi ya mila na desturi ambazo watu
wamezishikilia ambazo ni kikwazo katika mapambano dhidi ya mimba na ndoa za
utotoni, kuna familia nyingine zina umaskini ambao nao unachochea tatizo kwani
familia zinaona watoto wa kike kama kitega uchumi chao,” alisema.
Nkinga (pichani) alisema kutokana na hali hiyo jamii bado inahitaji elimu
zaidi ili kupambana na ongezeko la idadi ya ndoa na mimba za utotoni na vitendo
vya ukatili wa kijinsia.
“Leo hii tunalalamika kuna mmonyoko wa maadili lakini
kiukweli suala hilo ni matokeo ya ukatili ambao wengi walifanyiwa wakati wa
utotoni.
“Takwimu zinaonesha kuwa watoto wanafanyiwa vitendo vya
kikatili lakini jamii haifuatilii, kwa mfano utafiti wa mwaka 2010 unaonesha
asilimia 39 ya wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 30 wanafanyiwa ukatili.
“Na kati ya watoto saba, mmoja anakuwa amefanyiwa ukatili, hivyo
tunahitaji ushirikiano wa karibu wa kila mmoja kufikisha ujumbe kwa mwenzake kwamba
hali ni mbaya,” alisema.
Naye Magreth Musai (mwenye MIC) alisema serikali iliona suala hilo
kuwa ni changamoto na kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwamo UNICEF
kutengeneza mpango kazi wa kitaifa wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia wa
miaka mitano.
“Awali kulikuwa na mipango nane ambayo tumeipitia kwa
pamoja na kutengeneza mpango mmoja na lengo ni kutokomeza ndoa na mimba za
utotoni na ukatili wa kijinsia, tutauzindua wakati wowote kuanzia sasa,”
alisema.
Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Maria Karadenizli akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na
kuomba ushirikiano wa serikali pamoja na vyombo vya habari ili kutengeneza mpango
mkakati wa kuondoa vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
Usia
Nkhoma Ledama kutoka UNICEF akieleza jambo wakati wa semina kwa waandishi wa
habari iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN) na
kuwakutanisha wadau mbalimbali wa serikali na kijamii iliyofanyika katika
Hoteli ya Double Tree jijini Dar Es Salaam
Pedro Guerra kutoka UNICEF akizungumza jambo katika semina
iliyowahusisha waandishi wa habari ili kuweza kuripoti habari za kijinsia hasa
za ukatili wa mama na mtoto.
Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN WOMEN) Lucy Tesha akizungumza jinsi shirika
hilo lilivyoweza kupambana na unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto wa kike
Baadhi
ya waandishi wa habari wakichangia mada inayohusu ukatili wa mama na mtoto
katika semina iliyofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa
habari wakiwa kwenye semina.
Ruth Ayisi kutoka UNICEF akitoa ufafanuzi kuhusu njia
wanazoweza kuzitumia waandishi wa habari kuripoti habari za unyanyasaji
wa kijinsia kwa mama na mtoto.Baadhi ya waandishi wakijadiliana
Chapisha Maoni