NA OMR - DAR ES SALAAM
SHULE ya Sekondari ya Almuntazir iliyopo Upanga jijini Dae es salaam imetozwa faini ya
Sh. milioni 25 kwa kosa la uchafuzi wa mazingira kwa
kutirirsha maji taka ya chooni katika mto msimbazi ndani eneo la mikoko katika
eneo la daraja la salenda na kujenga uzio wa ukuta bila kuzingatia mita sitini
zinazotakiwa kisheria.
Faini hiyo
inatakiwa kulipwa ndani ya wiki moja imetokana na ziara ya Naibu waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina iliyofuatia
malalamiko ya wakazi wa Upanga iliyompelekea Naibu Waziri kufanya ziara
yakwenda kujionea uchafuzi huo.
Akiongea kwa Niaba
ya shule meneja wa shule hiyo, Serialis Rwechungura amesema kuwa, watalipa
faini hiyo kama ilivyoelekezwa na serikali na hakuwa tayari kuongelea swala la
ukuta wa shule hiyo.
Naibu Waziri
Mpina amesisitiza kuwa serikali haitakuwa tayari kuwavumila wawekeajia
wakiukaji wa sheria hasa ya mazingira, na kuweka rehani maisha ya watanzania.
Aidha Naibu
Waziri (anayehojiwa hapo juu) alitembelea maeneo ya mwenge kijijini na kuonea uchafu wa
mazingira uliotokana na kuvuja kwa maji taka ya choo kutoka kwenye miundombinu
ya majitaka ya DAWASCO hali inayosababibsha wakazi na wafanyabiashara wa maeneo
ya mwenge kushindwa kustahimili hali hiyo na kuwa hatarini kupata magonjwa ya
maambukizi kama kipindupindu na homa ya matumbo.
Akiikemea DAWASCO
kwa mara nyingine kwa kutokuonyesha uwajibikaji na utii kwa mamlaka za juu,
Naibu Waziri Mpina ameita NEMC kuiandikia DAWASCO faini ya Sh. milioni
25 kwa kutelekeza miundombinu yao na kutakiwa kulipa adhabu hiyo
kwa muda wa wiki mbili.
Chapisha Maoni