NA OMW, ZANZIBAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi wa Tanzania Zanzibar waache tabia ya kuwaoza wasichana wa kike wakiwa na umri mdogo bali wawasomeshe kwa ajili ya manufaa yao ya jamii kwa ujumla.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizindua madrasa ya kisasa iliyojengwa kwenye eneo la Kilimani na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa msikiti mkubwa kuliko yote nchini Tanzania unaojengwa katika eneo la Jitimai kidoti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa michango ya wananchi katika siku yake ya kwanza ya ziara ya Kikazi Kisiwani Unguja.
Makamu
wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan
akiweka jiwe la msingi katika ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul
Munawwaratul Islamiyyah ya Kilimanin Tazari Zanzibar ikiwa sehemu ya
ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesisitiza kuwa pamoja na elimu kuwa ni haki ya msingi kwa mtoto wa kike hivyo ni muhimu kwa jamii nzima ya Zanzibar ihakikishe watoto wa kike wote wanapata elimu kwani watakuwa na uwezo wa kuchagua na kuandaa mustakbali wa maisha yao ya baadaye ikilinganishwa na hali ilivyo sasa kwenye baadhi ya maeneo.
Makamu
wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan
akiangalia ramani ya msikiti mkubwa unaojengwa kwa nguvu za wananchi
alipotembelea Uwanja wa Jitimai uliopo Kidoti mkoa wa Kaskazini Unguja
Amesema vijana wengi wanaolelewa kwa kufuata misingi ya bora ya dini ni vigumu kurubuniwa na kujiingiza katika matendo yasiyofaa katika jamii.
Chapisha Maoni