NA VERONICA
ROMWALD – DAR ES SALAAM
VITENDO vya
mauaji kisha miili kutiwa kwenye viroba na kwenda kutupwa ama mtoni au
kutelekezwa mahali popote vimeibuka nchini.
Desemba 6,
mwaka huu kuliripotiwa tukio la aina hiyo, huko katika mkoa wa Pwani eneo la
Bagamoyo katika mto Ruvu.
Katika eneo
hilo wananchi walihisi uwepo wa harufu kali kabla ya kuona viroba vikiwa
vinaelea juu ya maji ambavyo walivitilia shaka.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba
Wakazi hao
wali baada ya kugundua miili
hiyo ikielea katika Mto Ruvu, walimpigia simu Mwenyekiti wao wa Kitongoji cha
Mtoni, Maneno Mafumba ambaye alifika kujionea tukio hilo.
Mwenyekiti
huyo alifika hapo akiwa ameongozana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Bagamoyo,
OCD Maro wakiwa wameambatana pia na madaktari wa Hospitali ya Bagamoyo.
OCD huyo
aliamuru miili hiyo kuopolewa lakini haikuchunguzwa kwa madai kuwa ilikuwa
imeharibika vibaya na hivyo ikaamuriwa izikwe, jambo ambalo lilitushangaza
wengi na kutuacha na maswali.
Kwamba kwanini
haikuchunguzwa kujua kama watu hao waliuwawa kwa sumu au la maana wengi wanahisi
kuwa huenda waliuwawa kwa njia hiyo, tunashukuru ilifukuliwa kwa ajili ya
uchunguzi ingawa bado miili hiyo haijtambulika hadi sasa.
Zikiwa
zimepita siku chache tu tangu kutokea kwa tukio hilo, mwili mwingine umekutwa
tena ukiwa umefungwa kwenye kiroba na kutelekezwa katika eneo moja huko mkoani
Kilimanjaro.
Kwa kuwa
wananchi tulipaza sauti kuhoji sababu za kutochunguzwa kwa vifo vya watu wale
saba ambao Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisikika akisema
kwamba huenda ni ya wahamiaji haramu.
Tumeshuhudia
awamu hii mwili uliokutwa huko Kilimanjaro ukiwa umechukuliwa kwenda kufanyiwa
vipimo kabla ya kuzikwa.
Si lengo la
makala haya kuhoji kauli ya Waziri Mwigulu jambo ninalotaka kueleza hapa ni
kuhusiana na mauaji haya yalioanza kutokea hapa nchini.
Nia yangu ni
kuvihimiza vyombo vya dola kutokufumbia macho vitendo hivi kusudi visije
vikashamiri katika nchi yetu.
Kwamba
tusiishie kusema wale walikuwa wahamiaji haramu kasha tukakaa kimya pasipo
kuchukua hatua za ziada za kuimarisha mifumo yetu ya ndani.
Hapa vyombo
vya dola visiachwe vifanye kazi peke yake, jamii inapaswa pia kushirikishwa.
Wakati fulani
nilipata kusoma makala ya mwandishi mmoja ambaye ni mkongwe kidogo katika fani.
Mwandishi huyo
alikuwa akieleza juu ya mfumo wa nyumba kumi ulivyokuwa ukifanya kazi na
ambavyo ulisaidia kuimarisha ulinzi wan chi kuanzia huko majumbani.
Leo hii utaona
jinsi ambavyo tunashindwa kuimarisha ulinzi wetu kwa sababu hata huko mitaani
wengi hatujuani.
Utamkamata
nani umwambie kuwa ni mhamiaji haramu hata hao wajumbe wa nyumba kumi baadhi
yao hawawajui watu wanaoishi kwenye mitaa yao.
Hakuna
utaratibu mzuri wa kuwatambua, ingawa kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa mfano
nilipata kumsikia mkuu wa mkoa Paul Makonda akiwaagiza kuhesabu watu wanaoishi
katika kila nyumba.
Lakini katika
eneo ninaloishi binafsi sijaona jambo hilo likitekelezwa, sijui kama maeneo
mengine viongozi walitii agizo hilo.
Ni wakati wa
kuamka na kufanya ufuatiliaji kusudi iwe rahisi kubaini mambo kabla matukio
hayajatokea katika nchi yetu.
Chapisha Maoni