Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMWDwJ0eOhPmwJUZVKTfCSnCelGl8z_LEh_kqsNqC9yN60YUKKteczqdOh9fMSNQfSnQ-Ajl-KsTWfbQAAl4nMvtP20Hys8e3RlmL1qWyHSFkc_jCliVT0JysM6TJCDPF9ZPtY0kbe2rC5/s1600/Bukuku.jpgNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

Mpigapicha maarufu Mpoki Bukuku amefariki dunia leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma (MOI) Almas Jumaa.

http://cache.saahiihii.com/images/340_340imagesstorySWTBusiness1397PICTURE1.jpg"Ni kweli Mpoki amefariki dunia mchana huu, alipokelewa jana usiku baada ya kupata ajali ya gari maeneo la Mwenge ITV, taarifa zaidi tutazitoa baadaye," alisema Almas. 
Taarifa zinasema marehemu alikuwa ametoka kazini jana usiku, akagongwa na gari maeneo ya Mwenge na kuvunjika miguu yote miwili na mkono mmoja. 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh6POVA2vYIlf3ovRh_UvEVslEenUfsZyw5TEwRPT-2EMMyYsG8-fLRZf8jCrcd_pIpdV1pmSRqa1GBdIFWWePU7wErHkbMEbVFJeaMVflv5os6mfnx_yPZU6v9G-xt5Im8kSDSSeZaZ9Q/s1600/DSC_0906.JPGMpoki Bukuku amewahi kufanya kazi kama Mpiga Picha Mkuu katika gazeti la Mwananchi, linalochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti. Pia amewahi kufanya kazi magazeti kadhaa likiwemo Majira na Nipashe.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiB52YynewH0-iOxXqCZg0x1otSfjymkX_nlFfYJpqrUohZkMLOTUn2IRzA4gQ7eu5LH0BpFx-XQYldYw7HgSQPcM_cDb5I1J8I3-D1Fg_obNi6QeBvNh8zxmI6iuC1anUbmildWGKzDpY5/s400/2.jpeg
Blog ya matukionamaisha inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki,

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Amen.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement