Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

RIPOTI ya utafiti uliofanywa na uwezo (iliyopo Twaweza) imeeleza kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya matokeo ya kujifunza na utapiamlo.

Utafiti huo ulilenga kuangalia juu ya uhusiano uliopo kati ya lishe na matokeo ya kujifunza,ulifanyika kati ya Oktoba na Desemba, mwaka jana.

Uwezo ilitoa matokeo ya utafiti huo Dar es Salaam jana katika halfa iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akizungumza kuhusu utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema ulihusisha watoto 197,451 na kaya 68,588 nchini. 
 balanced diet
“Matokeo yanaonesha miongoni mwa watoto wenye miaka 10 mpaka 14, ambao walipimwa uwezo wa kusoma hadithi ya kingereza ya kiwango cha darasa la pili, Watoto wenye utapiamlo walifaulu kwa kiwango cha asilimia 17.9, wenye utapiamlo wa wastani asilimia 16.4 na wasio na utapiamlo walifaulu kwa asilimia 25.8.
 
“Walipimwa pia uwezo wa kusoma hadithi ya Kiswahili ya kiwango cha darasa la pili ambapo watoto wenye utapiamlo walifaulu kwa asilimia 46.3, watoto wenye utapiamlo wa wastani asilimia 51.3 walifaulu na wasio na utapiamlo asilimia 65.8 walifaulu,” alisema.

Aliongeza “Walipimwa uwezo wa kufanya hesabu za kuzidisha za kiwango cha darasa la pili, watoto wenye utapiamlo asilimia 35.5 walifaulu, watoto wenye utapiamlo wa wastani asilimia 37.7 walifaulu na wasio na utapiamlo asilimia 53.4 walifaulu.

“Matokeo haya yanaonesha watoto wasio na utapiamlo wanafaulu zaidi kusoma masomo ya Kiswahili na Hisabati kuliko wale wenye utapiamlo,” alisema.
 http://pool.hesperian.org/w/images/thumb/c/c6/SW_NWTND_Nut_Page_20-3.png/350px-SW_NWTND_Nut_Page_20-3.png
Alisema takwimu zilizokusanywa zinaonesha kuwa, kwa ujumla kitaifa, asilimia nne ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, asilimia 5.6 ya watoto wenye miaka kati ya mitano na tisa na asilimia 5.7 ya watoto wenye miaka kati ya 10 hadi 14 wana utapiamlo.

“Hata hivyo kuna utofauti mkubwa kiwilaya, asilimia 23.9 ya watoto wa Songea Mjini walio chini ya miaka mitano wana utapiamlo ukilinganisha na asilimia 0.3 wilaya ya Tabora Mjini na Musoma Mjini,” alisema.

Alisema kwa wastani, asilimia 50 ya kaya zinamudu milo mitatu kwa siku. 

“Matokeo yanaonesha kuwa baadhi ya wilaya zina zaidi ya asilimia 85 ya kaya zinazomudu milo mitatu kwa siku, Mbulu asilimia 97.6, Kishapu asilimia 88.2, Mafinga Mjini asilimia 88, Tunduma asilimia 86.4, Moshi Mjini asilimia 86. Lakini katika wilaya nyingine, kaya chini ya asilimia 40 ndizo zinazomudu milo mitatu kwa siku mfano Masasi asilimia 38.6, Tandahimba asilimia 35.5, Mtwara Vijijini asilimia 27.6 na Nanyumbu asilimia 23.1,” alisema.

Alisema kitaifa,  ni shule moja tu kati ya tano inayotoa huduma ya chakula cha mchana shuleni sawa na asilimia 23.

Alisema kwa mkoa wa Kilimanjaro asilimia 79  ya shule zinatoa chakula cha mchana lakini katika mkoa wa Geita, ni asilimia tano tu ya shule zinazomudu chakula cha mchana kwa watoto.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjD3GTDPyQe19GZmIQhRnDHAO6P8IrtGUekXOGB2YWivR5IQLxkl0cwS7JouTeHyGGMNI80jw5FsBCL1iS5dikBsHITJKOkvGdUj0fmMcGUFKS5Siyj4ypvpCIjnw0KNTqUDTTttv0D_Q0w/s640/LISHE.jpg
“Utafiti huu umethibitisha kile ambacho wengi wetu tulikuwa tunadhani, uwezo wa watoto kufanya vizuri shuleni unaathiriwa na jinsi wanavyopata lishe nzuri. 

“Katika awamu hii ya elimu bila malipo ya ada, suala la utoaji wa chakula shuleni limeachwa njia panda. Halijaainishwa kwenye fedha za ruzuku zinazotumwa moja kwa moja shuleni na serikali. 

“Wazazi nao wameacha kutoa michango shuleni, kutokana na matamko rasmi ya kufuta michango yote mashuleni. Tunajiuliza, Je, suala la michango ya wazazi kwa ajili ya chakula cha watoto wao waki shuleni bado halizungumziki?  Si vibaya tukalijadili hili pia, miongoni mwa jitihada nyingine sinazofanywa kuhakikisha watoto wetu wanajifunza,” alisema.

Meneja wa Uwezo Tanzania, Zaida Mgalla, alisema takwimu hizo zinaonesha taswira ya hali ya lishe ya watoto. 

“Inaonekana wazi kwamba upo uhusiano mkubwa kati ya lishe ya watoto na matokeo yao ya kujifunza, hivyo utoaji wa chakula shuleni inaweza ikawa njia mojawapo ya kuwapa motisha wanafunzi kuhudhuria zaidi shuleni,” alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement