Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2015/12/pingu.jpgNA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MZAZI mchunge mwanao, ndiyo ujumbe mahususi unaopaswa kuusimamia kuelekea sikukuu ya christmass na mwaka mpya.

Unatakiwa kuwa makini kwani Jeshi la Polisi nchini limeonya kwamba litawachukulia hatua kwa kuwakamata na kuwashtaki wazazi wa watoto ambao watapotea na kufikishwa katika vituo vya polisi.

Msemaji wa Jeshi hilo, Kamishna Msaidizi, Advera Bulimba (pichani chini), ameeleza hivyo katika mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya jana Dar es Salaam.

Amesema imekuwa ni kawaida kwa watoto wengi kufikishwa vituoni baada ya kupotea katika kipindi cha msimu wa sikukuu.

“Tutawaita wazazi watusaidie wakati watoto wanapotea wao walikuwa katika mazingira gani, maana imekuwa ni kawaida kipindi cha sikukuu vituo vya polisi vinajaa watoto waliookotwa katika maeneo mbalimbali, ikiwamo fukwe za bahari,” alisema.
  https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiaLec8BJAtLioGhha-7uFzfx4rnpgcqCNdj4BI5fm36EoRYacAyh6538NGAeUh6s1JKDC4jr087EemeZuHMlI2fq7TzAZcSV_Qd97Dh9RDyFfsY5pc0Wdwk4rhhT7FuNLiq9r7sOicitVv/s1600/polisi.jpg
Aidha, aliwataka wananchi kuepuka kulewa kupita kiasi, hasa wale wanaoendesha vyombo vya moto na kwamba wakikamatwa sheria itachukua mkondo wake.

“Kwa ujumla wananchi wajue kwamba jeshi lao limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kuelekea msimu huu wa sikukuu.

“Uzoefu unaonyesha sikukuu za mwisho wa mwaka huambatana na vitendo vinavyohatarisha usalama wa raia na mali zao, utumiaji wa vilevi kupita kiasi, utapeli, wizi, unyang’anyi na uendeshaji wa vyombo vya moto bila kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, askari watafanya doria wakati wote,” alisema.

Aliwataka pia watu wanaomiliki nyumba za kulala wageni na maduka makubwa kama vile hoteli na ‘supermarket’ kufunga kamera za usalama.
 https://i.ytimg.com/vi/9PmA7XvGvhk/sddefault.jpg
“Wafunge kamera ili waweze kufuatilia kila kinachoendelea katika maeneo yao, nani kaingia, nani katoka na anafanya nini,” alisema.

Pia, aliwaonya wafanyabiashara wanaomiliki kumbi za starehe, huku likiwataka kuzingatia masharti ya leseni zao walizopewa hasa msimu huu wa sikukuu.

Amewataka wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie kiwango cha idadi ya watu wanaoruhusiwa kuingia ukumbini na iwapo watagundulika kuzidisha watachukuliwa hatua kali za kisheria.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiF-ypMKHUBE1iY6Q0-RN25pq3Bv_drVTQn8301IFobGE6NNWDrJqBgsVlhEce3qQIaQJLKjbtTMiYCqBxwCKb-pOx73ErbMwY8kPEgJGTiVLH_YV041-gg4GH4EJjUG4GpPJeWCJQhERCu/s320/jeshiiii+la.jpg
“Tumegundua katika msimu wa sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kuitumia fursa hiyo kujipatia kipato kisicho halali.

“Tutapita hadi kwenye kumbi za starehe, tukikuta mtu ameruhusu watu zaidi ya kiwango cha leseni yake tutamchukulia hatua za kisheria,” alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement