Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Image may contain: 1 personNA ALVIN DAUDI, MAELEZO

WATAALAMU wa afya wametakiwa kutumia utaalamu na wajibu wao katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi kwa ajili ya kujenga taifa lenye kizazi imara.
 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Pichani juu) wakati wa ufunguzi wa mkutano katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa huduma za afya ya uzazi na mtoto uliofanyika Mkoani Dodoma.  Image may contain: 4 people, people sitting
Watumishi wa afya wakimsikiliza Waziri Ummy katika mkutano huo

“Tumieni utaalamu wenu na wajibu mliopewa kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi katika kuboresha afya ya uzazi na mtoto” alisema Waziri Ummy.
 

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wataalamu na wasimamizi wa huduma za afya ya uzazi na mtoto, wana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya, kwa kuhakikisha kuwa, huduma zinaboreshwa zaidi na kutolewa kulingana na viwango vilivyowekwa.
 

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga imeendelea kuwa juu. 
 Image may contain: 3 people, people sitting and indoor
Mathalani, vifo vitokanavyo na uzazi mwaka 2010 vilikuwa vifo 454 kwa kila vizazi hai 100,000 na mwaka 2015 viliongezeka hadi vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000.
 

Aidha Waziri Ummy alisema kuwa kiwango cha vifo vya watoto wachanga kimeendelea kupungua kwa kasi kidogo kwani mwaka 2010 vilikuwa vifo 26 kwa kila vizazi hai 1,000 na mwaka 2015/16 vilipungua hadi kufikia vifo 25 kwa kila vizazi hai 1,000 .Image may contain: 1 person
Aidha Waziri Ummy alisema kuwa kiwango cha vifo vya watoto wachanga kimeendelea kupungua kwa kasi kidogo kwani mwaka 2010 vilikuwa vifo 26 kwa kila vizazi hai 1,000 na mwaka 2015/16 vilipungua hadi kufikia vifo 25 kwa kila vizazi hai 1,000 .
 

Waziri Ummy alisema kuwa yapo maendeleo yanayotia moyo kwa upande wa kupungua kwa kiwango cha vifo vya watoto walio na umri chini ya miaka mitano kutoka vifo 112 kwa kila vizazi hai 1,000 hadi kufikia vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2015/16.  Image may contain: 9 people, people standing and shoes
“Tumeweka baadhi ya mikakati ikiwemo kujengea uwezo vituo vya afya ili viweze kutoa huduma za dharura za upasuaji wa kutoa mtoto, kuhamasisha wanawake kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora wakati wa kujifungua” alisema Waziri Ummy.
 

Mkutano huo wenye lengo la kujadili mafanikio na mikakati ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kuboresha Afya ya Uzazi, Vijana na Watoto (One Plan II) umebeba kauli mbiu isemayo “Kutoa Taarifa na kufanya Mapitio ya Vifo vitokanavyo na Uzazi na Vifo vya Watoto wachanga; ni jukumu letu sote, Tuwajibike”.


Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement