Dar es Salaam
Kwa mara ya kwanza, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeanza
kuuza nje ya nchi bidhaa zake katika soko la kikanda.
Eneo la kwanza likiwa ni nchi jirani ya Tanzania
kwa upande wa Kaskazini, Kenya.
Shehena ya kwanza ya bia inayofahamika kama
Allsopps ilisafirishwa kwenda Kenya wiki iliyopita na hivyo kukiweka kiwanda
cha SBL kuwa mmoja wachangiaji wakubwa katika soko la kanda.
Akizungumzia kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
SBL, John Wanyancha alisema; “Hii ni hatua nyingine ya
kufurahisha katika kampuni yetu na kimsingi
kwa bidhaa zetu.
Ukweli unabakia kwamba kumudu kupenyeza ndani ya
soko la Kenya kunaonesha kuwa ubora wa bidhaa
zetu sio tu kwamba unakubalika na wateja wetu wa ndani
bali pia zinakubalika katika soko kubwa la
kikanda.”
Wanyancha alisema kuwa SBL inaangalia uwezekano wa
kupanua mauzo ya biashara katika masoko mengine ya kikanda, hatua ambayo
iko katika mkondo wa kuhamasisha Jumuia ya Afrika
Mashariki na kada nyingine za kiuchumi kuongeza biashara
yake ya kuvuka mpaka ndani ya ukanda huo.
SBL imekuwa inazalisha aina za
bidhaa zinazotambulika kimataifa kama vile Pilsner
Lager,Tusker Lager, TuskerLite, Kibo Gold, Guinness Stout, Uhuru, The Kick
pamoja na bidhaa kuu ya Serengeti Premium Lager-ambayo peke
yake imeshajizolea medali kumi zinazotambuliwa kimataifa.
Chapisha Maoni