Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
NA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM

“Naikumbuka vema siku aliyonifuata na kuniambia ananipenda na yupo tayari kuishi na mimi maisha yake yote, sikusita kumkubalia kwani nilihisi damu zetu zilikuwa zimeendana, nilimkubalia”

Ndivyo alivyoanza kujieleza, Neema Mwita mkazi wa Mara mkoani Musoma alipozungumza na (MATUKIONAMAISHA)- MTANZANIA wodini alipolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Tofauti na siku zingine za nyuma ambapo alionekana kuwa mwenye huzuni, awamu hii  Neema alikuwa mwenye furaha wakati wote alipokuwa akizungumza na mwandishi wa makala haya.


Neema anaendelea kusimulia “Alilipa mahari iliyotakiwa nyumbani kwetu na tukapewa baraka na wazee, tukafunga ndoa kanisani, nakumbuka siku ile jinsi tulivyokuwa tukitembea kwa unyenyekevu kuelekea madhabahuni.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYlH9NqkdrZRj75bcZCNyiEBYbwL1guAiAApgHjWVCw1ebJIqTPjqVQsrZuWmSIhppnm6tA5WBR-g_GyhusRhe6WbSvHEVE-wdCi-Y2dejBbCnwX61kt4jmLOtc9VAY8F4twZyafCH8vQt/s1600/ima++ges.jpg “Lakini, sikuwahi kufikiri ipo siku atabadilika tabia na kunisababishia matatizo makubwa kwenye maisha yangu niliyonayo hii  leo,” anasema.

Akiendelea kusimulia Neema anasema walijaliwa kupata watoto watatu katika ndoa yao.


Jinsi ilivyotokea


“Siku moja nikiwa na mimba ya miezi mine, niliingia shambani nikachuma mahindi mawili ili nile na wanangu maana nilikuwa nahisi njaa sana, nikakaa kwenye kigoda baba alikuja akanihoji kwanini nilichukua mahindi na nilichukua wapi.

https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEh4F7d2G3BZwBEGF37cEqtkSxT3r0ahYbxkTJeEiAQRC1_dr1d99cqb_eQdj92-iyHq1g_pMtrmtdJYeERaC2yme-l778hwegih83x0tQHXkFjOr6TfYrAUmHTGikkQrHhRmJ5Jbi20qxw0p4HuB_CHZF4IodpcxpptxZ9UtMuR7BnXA8gFOv4hrSDYQmY1q0bUkDo4TCKxJc0AYSc284ZPKkIgRvapX1fsUA=w1200-h630-p-k-no-nu “Akaniambia ngoja nije nikusaidie kuchoma mahindi, akatoka nje nikajua kweli anakuja kunisaidia lakini aliporudi alianza kunipiga,
akanidondosha chini alichukua maji jikoni na kunimwagia yaliniunguza kifuani, akanifungia ndani,” anasema.


Anasema hata hivyo mtoto wake mmoja alikuwa akimpatia chakula hasa uji kwa kuingia ndani ya chumba hicho kwa siri.


“Baadae nilipata wasamaria wema wakanisaidia nikaondoka kwenda Musoma, lakini kadri nilivyokaa nyama ya kifua na shingo zilikuwa zikiendelea kushiakana, siku moja alikuja Joyce Kiria akanionea huruma jinsi alivyoniona,” anasema.


Anasema pamoja na mambo mengine aliyomsaidia, Kiria alimnunulia simu na kumuunganisha na watu ambao waliweza kumsaidia fedha na hivyo kuanza matibabu.


Neema anasema hawezi kusahau tukio hilo lilitokea miaka miwili iliyopita kwani limemsababishia jeraha kubwa katika maisha yake.

 
“Nilikuwa naumia, nilikuwa nikijikuna navimba, ilifika mahali sauti ilikuwa inakwama kutoka, watu waliendelea kuwasiliana na mimi, hadi
Rais John Magufuli alipopata taarifa zangu na kunisaidia, naamini kwa uwezo wa Mungu nitapona,” anasema.


Ndugu walimtenga

 
“Tangu wakati huo hadi leo sijui huyo baba alikimbilia wapi na hajarudi kijijini hadi leo, baadhi ya ndugu zangu waliogopa kunisaidia
na hata kunichukua nikae nao.


“Walihofu kwamba huenda siku moja angerudi sasa kama asingenikuta ingeleta matatizo mengine, kwani alikuwa amelipa mahari nyumbani kwetu, na kule (kijijini) mahari inaheshimiwa,” anasema.

http://www.emat.or.tz/uploads/8/9/2/7/89274330/screen-shot-2013-07-22-at-3-01-26-pm-1.jpg?565 Safari ya matibabu ilivyokuwa
Daktari Bingwa wa Upasuaji na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Muhimbili, Ibrahim Mkoma anasema wamemfanyia upasuaji awamu tatu mama huyo hadi sasa.


“Alijeruhiwa vibaya, maji yale yalipenya hadi kwenye mifupa yake katika baadhi ya sehemu za mwili wake na kumsababishia ulemavu.
 

“Awamu ya kwanza ya upasuaji tulitenganisha nyama zilizokuwa zimeungana kati ya mkono na shingo, kisha tulichukua ngozi katika sehemu ya paja na kujaza sehemu ambazo hazikushikana vizuri.

“Lakini alikuwa bado anahisi maumivu makali, akarudi tena hospitalini tukamfanyia upasuaji kwa awamu ya pili, tulichukua ngozi kwenye tumbo
lake na kujaza katika maeneo ambayo hazikushikana,” alisema.


Anasema walimfanyia tena upasuaji awamu ya tatu kwa kushirikiana na madaktari wenzao waliotembelea nchini wa Ujerumani na Uswizi.

http://www.bongomovies.com/wp-content/uploads/2017/02/RAIS-MSAADA.jpg “Lakini afya yake haikuwa nzuri, awamu hii tuligundua alikuwa amepatwa na tatizo kitaalamu tunaita ‘Post traumatic stress disorder’, hujitokeza kama matokeo ya mtu kupatwa na tatizo kubwa,
tukawashirikisha wataalamu wa saikolojia, viungo na mifupa kumpatia matibabu na sasa hajambo kabisa,” anasema.


Tumaini larejea

Neema anasema alikuwa amekata tamaa ya maisha na alitamani kujiua.


"Waliniambia nitakufa siku yoyote... muda wangu wa kuishi si mrefu tena, nilitamani ninywe hata dawa nijiue lakini nashukuru Mwenyezi Mungu hadi leo nipo na afya yangu imeimarika, sisikii tena yale maumivu niliyokuwa nasikia, naamini ni mapenzi yake.

Ahadi yake kwa JPM

"Namshukuru Rais Magufuli amenisaidia mno, nitaendelea kumuombea hadi nitakapoondoka duniani, nimejulishwa pia kwamba wanangu wameshapelekwa shule kama alivyoniahidi,” anasema.


Atamani kuwa mjasiriamali

"Pindi nitakapotoka hapa hospitalini natamani niende kuishi Mwanza, kwani kuna fursa nyingi za kibiashara. Nataka niwe mjasiriamali, pale kuna ziwa iwapo nitasaidiwa kupata mtaji ninao uwezo wa kufanya biashara ndogondogo kwa mfano kuuza samaki au nikafungua kibanda changu cha biashara nikauza bidhaa mbalimbali,” anasema.
 

Neema anasema hawezi kufanya kazi ngumu kama vile kulima kwani baada ya mkasa ule amepata ulemavu wa kudumu.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement