Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

http://jkci.or.tz/uploads/gallery/large_1473174606-jengo%20croped.jpgNA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MADAKTARI wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji mkubwa wa kubadilisha milango zaidi ya miwili ya moyo iliyokuwa imeziba.

Upasuaji huo umefanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki hospitalini hapo, Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa (katikati) alisema kambi hiyo ya upasuaji ilianza Machi 26, mwaka huu na kuisha jana.

“Tumefanya pia upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika milango ya moyo iliyokuwa imeziba. Upasuaji huu kitaalamu unaitwa ‘Coronary Artery Bypass Graft’ tumewafanyia jumla ya wagonjwa wanane,” alisema.

Dk. Nyangassa alisema katika kambi hiyo wamefanikiwa kumfanyia upasuaji mtoto mwenye umri wa miaka minane ambaye mshipa wake mmoja ulikuwa umesinyaa.

“Pamoja na hao tuliwafanyia upasuaji watu wazima wanne ambao walikuwa wana matundu kwenye moyo," alisema.
Mmoja wa wagonjwa aliyefanyiwa upasuaji huo, akitoa shukruni zake.

Naye  Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa JKCI, Dk. Peter Kisenge, alisema kwa mara ya kwanza waliweza kuzibua mlango wa moyo ambao hupitisha damu isiyo na hewa ya oksjeni kuipeleka kwenye moyo mbao ulikuwa umeziba.

“Tumewafanyia upasuaji bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa ‘cath lab’ wagonjwa 12 ambao mishipa yao iliziba kwa asilimia 100, mgonjwa mmoja tumemuwekea betri ya pacemaker,” alisema.

Alisema tangu Januari, mwaka huu hadi Machi taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wan je ya nchi wamefanya
Mwenyekiti waMadhehebu ya Bohora nchini, Zainudi Adamjee akizungumza na waandishi katika mkutano huo.

Adamjee alisema kambi hiyo imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtakatifu, Dk. Syedna Aliqadr Mufaddal alipokutana na Rais John Magufuli Oktoba, mwaka jana nchini.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement