Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Image may contain: 11 people, people standingBujumbura, Burundi


Nchi wanachama wa Umoja wa Afika mashariki pamoja na sektarieti ya umoja huo(EAC) wamehimizwa kuharakisha mchakato wa kuhakikisha kada zingine za afya ikiwemo ya uuguzi na kada nyingine zenye sifa na viwango vinavyofanana na madaktari kuajiriwa kwenye nchi yeyote ya Afrika Mashariki.
Image may contain: 3 people, people smiling, people standing, people sitting and indoor Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kisekta la mawaziri wa Afya wa Afrika mashariki amesema hayo mapema leo kwenye kikao cha 14 nchini hapa.

Waziri ummy ameeleza kufurahishwa mno na hatua iliyofikiwa na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Kikao hicho kimejadili pia juu ya kuimarishwa kwa mafunzo na usimamizi wa pamoja wa wataalam wa afya, udhibiti wa magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa ya kuambukiza kama vile ebola, mafua makali ya ndege kifua kikuu(TB) na UKIMWI.
Image may contain: 5 people, people sitting and indoor Kuhusu kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto, mawaziri hao wamekubaliana kuongeza juhudi zaidi ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto ndani ya Afrika Mashariki.

“Bado Afrika Mashariki hatufanyi vizuri katika afya ya uzazi na mtoto na hivyo kusababisha kutofikia malengo ya kidunia ya Millenia yaliyowekwa, hivyo tuongeze jitihada katika hili," amesema Waziri Ummy.


Aidha, ameielekeza Tume ya Utafiti wa masuala ya Afya ya EAC ihamie mapema makao makuu yake mjini hapa kama ilivyokubaliwa kwenye vikao vya baraza la mawaziri vilivyotangulia.

 Image may contain: 3 people, people sitting
Wakati huo huo Waziri Ummy akiwa nchini humo ameshiriki uzinduzi wa kongamano la Kimataifa la afya ya Sayansi lililofunguliwa na Rais wa Burundi Piere Nkurunzinza.

Kongamano hilo la siku tatu limeandaliwa na Kamisheni ya Utafiti wa Masuala ya Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Limelenga kujadili na kujipanga katika kukabiliana na majanga ikiwemo ya magonjwa mapya yanayojitokeza(Emerging Diseases) na yale yanayojirudia (Re-emerging Diseases) na linawawashirikisha wataalam wa afya na watafiti kutoka nchi mbalimbali.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement