Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Image may contain: 3 people, people standingNa Catherine Sungura, W. Afya-Dodoma

KITABU cha Maapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria kimezinduliwa leo mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ndiye aliyezindua rasmi kitabu hicho.

Amesema takwimu kutoka katika vituo vya kutolea huduma za Afya zinaonesha kuwa, takribani wastani wa watu million 12 huripotiwa kuwa na ugonjwa wa malaria katika vituo vya kutolea huduma za Afya kwa mwaka nchini.
 
"Siku ya Malaria Duniani, huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 25 mwezi April, kila mwaka, lengo kuu la maadhimisho haya ni kuielimisha na kuikumbusha jamii ili kutambua athari za ugonjwa wa malaria, jinsi unavyoambukizwa, na namna ya kujikinga," amesema.

Amesema maadhimisho hayo pia hutumika kuihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua dalili za malaria mapema; 
 Image may contain: 6 people, people standing
"Ni vema mwananchi awahi kituo cha kutolea huduma za afya ili kupima na kuthibitisha uwepo wa vimelea vya malaria kabla ya kuanza kutumia dawa, tumia dawa sahihi ya kutibu malaria pale itakapothibitika kuwa na vimelea vya malaria na kukamilisha matibabu ya malaria kulingana na maelekezo ya mtoa huduma," amesema.

Amesema kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Shiriki Kutokomeza Malaria Kabisa, kwa Manufaa ya Jamii”.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement